MNAOCHUKUA FOMU JIPIMENI WENYEWE KWA AJILI YA WATANZANIA AU KWENDA KUPIGA PICHA BUNGENI

"Umechukua fomu kwa ajili ya watanzania, au unataka kupiga picha bungeni?" – Steve Nyerere Ahoji Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Mengele maarufu kama Steve Nyerere, ametoa kauli nzito kuhusu wimbi la vijana maarufu kuchukua fomu za kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025. Kupitia mahojiano maalumu, Steve Nyerere amewataka vijana hao kujiuliza kwa dhati: “Je, umechukua fomu kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania au unataka kupiga picha bungeni?” Ameeleza kuwa ni jambo jema kuona vijana wakijitokeza katika siasa, lakini akasisitiza kuwa siasa si jukwaa la kutafuta umaarufu au fursa za binafsi, bali ni wito unaohitaji moyo wa kweli wa huduma kwa wananchi. "Nafasi ya uongozi si ya kupigia picha bungeni. Ni wajibu, ni dhamana, na ni lazima uwe na moyo wa kweli wa kuwatumikia wananchi," amesema. Kauli hiyo imekuja katika kipindi ambacho kumeibuka wimbi la vijana wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kujitokeza kuchukua fomu ndani ya CCM, hali inayoibua mjadala kuhusu uhalisia wa nia zao katika kugombea nafasi za kisiasa. Steve amehitimisha kwa kuwasihi vijana hao kufanya tafakuri ya kina kabla ya kuingia kwenye siasa, ili kuhakikisha kuwa wanatoka na nia ya kweli ya kuleta mabadiliko, si kutafuta 'kiki'.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA