Posts

Showing posts from February, 2025

MSAMA POLE SANA WAZIRI MCHENGERWA

Image
Mkurugenzi wa Msama Promotion ameenda kutoa faraja kwa Waziri wa Tamisemi Mh Mchengwerwa kwa kafiwa na baba yake.

MSHINDI WA BSS KUONDOKA NA MAMILIONI

Image
  FINALI y a Shindano la Kusaka vipaji nchini Bongo Star Search (BSS) linatarajia kufanyika February 28, 2025 katika ukumbi wa Wareouse uliopo Masaki jijini Dar es Salaam. Mshindi wa kwanza kuondoka na kiasi cha Sh Milioni 20 , mshindi wa pili Milioni tatu na mshindi wa tatu Milioni moja. Akizungumza na Spotileo Chief Judge na Mkurugenzi wa Benchmark Madam Rita Paulsen amesema  kuelekea fainali ya bongo Star Search  msimu wa 15 inayotarajiwa kupandisha washiriki Sita kutoka nchini Tanzania, Uganda na nchini Demokrasia ya Congo. "Msimu huu kumekuwa wa tofauti na misimu mingine yote iliyopita kama mnavyojua tunawashiriki wa nje kwa sasa tumefanya Afrika na Mataifa mbalimbali walioingia hatua ya fainali. "Huu ulikuwa msimu ambao tulikusanya wasanii wa Afrika MasharikiHaikuwa kazi rahisi kufika tulipo, ushindani ulikuwa mkubwa, vipaji vilikuwa vingi lakini mwisho wa siku mtawashuhudia walioingia fainali hadi tutakapopata mshindi. Pia amefafanua kuwa Msanii Abiudi  kujito...

WAZIRI KABUDI AWATAKA WATANGAZAJI KUZINGATIA KISWAHILI

Image
  W AZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amewaonya watangazaji wa vyombo vya habari kuacha kubananga au kupotosha umma kuhusu Matumizi sahihi ya lugha Kiswahili. Akizungumza jijini Dodoma Leo kwenye Mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini uliondaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Professa Kabudi amesema baadhi ya watangazaji wamekuwa wakipotosha umma kwa kutamka matamshi yasiyo sahihi akitolea mfano apa badala ya hapa, uyu badala ya huyu na wengi huwafuata. "Tanzania tumefubaza Kiswahili kwa kudumaza kwa maneno kadhaa, kubananga Kiswahili matokeo yake watumiaji wengine wa nchi zinazotuzunguka wanaona hatuzungumzi kwa ufasaha,  "Watangazaji mna jukumu la kuhakikisha mnatangaza kwa lugha fanisi na fasaha. Vyombo vya Habari mna mchango mkubwa wa kusahihisha makosa mkiendelea hivyo, hilo ni janga litaigharimu nchi na kuacha kuwa  kinara"alisema. Amezitaka mamlaka zinahusika kuwachukulia hatua watangazaji ambao hawazinga...

MSAMA AWATA WASANII WA INJILI KUACHA KUIMBA JUKWAANI NA BONGO FLEVA

Image
Mkurugenzi wa Msama Promotions ndg Alex Msama Amewaonya waimbaji wote wa nyimbo za injili Ambao wamekuwa wakishiriki kwenye majukwaa na wasanii muziki wa kidunia, kwani kufanya ivo ni kushiriki kwenye kumtukuza shetani. Pia amewataka wasanii hao kuacha tamaa ya pesa ambayo inawapelekea wasanii hao kwenda kushiriki kwenye majukwaa ya muziki wa kidunia, “Nawaonya waache kushiriki madhabahu za shetani,2 Wakorinto 6: 14-18 Msiambatane pamoja na watu wasioamini, pia wajihadhari na kupenda pesa kwani pesa nyingine ni za maagano ya kuzimu” Alex MSAma Alex Msama ni mdau mkubwa wa Muziki wa Injili na Hivi karibuni alipokea tuzo ya heshima ya kuwa muandaaji bora wa matamasha ya injili nchini Tanzania ambayo maarufu yalikuwa yanafahamika kwa jina la TAMASHA LA PASAKA