MSHINDI WA BSS KUONDOKA NA MAMILIONI

 FINALI y


a Shindano la Kusaka vipaji nchini Bongo Star Search (BSS) linatarajia kufanyika February 28, 2025 katika ukumbi wa Wareouse uliopo Masaki jijini Dar es Salaam.


Mshindi wa kwanza kuondoka na kiasi cha Sh Milioni 20 , mshindi wa pili Milioni tatu na mshindi wa tatu Milioni moja.

Akizungumza na Spotileo Chief Judge na Mkurugenzi wa Benchmark Madam Rita Paulsen amesema  kuelekea fainali ya bongo Star Search  msimu wa 15 inayotarajiwa kupandisha washiriki Sita kutoka nchini Tanzania, Uganda na nchini Demokrasia ya Congo.

"Msimu huu kumekuwa wa tofauti na misimu mingine yote iliyopita kama mnavyojua tunawashiriki wa nje kwa sasa tumefanya Afrika na Mataifa mbalimbali walioingia hatua ya fainali.

"Huu ulikuwa msimu ambao tulikusanya wasanii wa Afrika MasharikiHaikuwa kazi rahisi kufika tulipo, ushindani ulikuwa mkubwa, vipaji vilikuwa vingi lakini mwisho wa siku mtawashuhudia walioingia fainali hadi tutakapopata mshindi.

Pia amefafanua kuwa Msanii Abiudi  kujitoa Kwenye mashindano hayo ambapo amesema alijitoa mwenyewe Sababu alikuwa na ishu binafsi na mpenzi wake..

Madam Rita amesema kuwa lengo la kuwapatia wasanii wachanga fursa ya kuonekana zaidi kwenye jamii na kuwawezesha kuwa mastaa wanaojipatia kipato.

Rita amewaimiza Wadau kumuunga Mkono katika Finali katika kumtafuta mshindi wa Mwaka 2024/2024.

Kiingilio kwenye Mashindano hayo kawaida ni kiasi cha Sh 20000 kawaida, kwa VIP 30000 na VVIP 50000.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA