Kuelekea Tamasha la Pasaka mwaka 2024 Alex Msama Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion mwaandaaji wa Tamasha hilo amethibitisha waimbaji wa muziki wa injili kutoka mataifa zaidi ya 8 watakuwepo kwenye Tamasha la Pasaka la mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari Alex Msama kuwa maandalizi makubwa kuelekea Tamasha hilo yamekwisha fanyika kwa asilimia kubwa na watu wakae mkao wa kula kwani Tamasha la mwaka huu litakuwa na zuri na lenye shangwe kubwa sana kwa wakazi wa mkoa wa Dar es salaam. Tamasha la mwaka huu litafanyika siku ya Jumapili ya Pasaka, huku kauli mbiu ikiwa ni ASANTE MUNGU KWA KUTUPA RAIS SAMIA S HASSAN MCHAPA KAZI
Wanandoa watashauriwa kuwa na mitoko ya pamoja kujua mwenzio anapenda kula nini kuvaa na kunywa ili kuendelea kudumisha ndoa yao, Ndoa bora ni ushirikiano, siyo mashindano. Akizungumza mwaandaaji wa Usiku huo wa wanandoa The Pinnacle of Mentorship & Excellence Award (PIMEA) Dkt Christine Mbelwa amesema Lengo la Usiku wa Wanandoa nikuwakutanisha na kubadilishana mawazo kuhusiana na kukumbusha baadhi ya mambo ya ndoa. "Moja ya majukumu ambayo Mungu amenikabidhi mimi pamoja na mume wangu ni kujenga ndoa na mahusiano imara kupitia uandishi wa vitabu, semina, makongamano na mafundisho mbalimbali. "Usiku wa Wanandoa ni moja ya jukwaa kuu tunalotumia kwa lengo la kuboresha, kuponya na kuokoa ndoa. Tunawakusanya wanandoa pamoja, kuwapa mafundisho ya vitendo ana kwa ana, kuruhusu maswali na kutoa majibu ya moja kwa moja. Amesema Zaidi ya mafundisho, wanandoa hupata nafasi ya kufurahi pamoja kwa kushiriki vinywaji, michezo na burudani mbalimbali. Shughuli hi...
"Ukosefu wa Fedha, Uongozi Dhaifu Vyatajwa Kuvuruga Uhai wa Taasisi za Vijana" Dar es Salaam. Ukosefu wa fedha, masharti magumu kutoka kwa wafadhili, kutokuwa na maarifa ya kutosha ya uendeshaji wa taasisi na rasilimali zake ni miongoni mwa changamoto zinazochangia taasisi nyingi zinazoanzishwa na vijana kufa kabla ya kufikia malengo yake. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Her Initiative, Lydia Charles, katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya uongozi kwa taasisi 20 zinazoongozwa na vijana kupitia programu ya Adaptive Leadership Program chini ya mradi wa Ustawi Lab. Amesema changamoto hizo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa vijana wanaotamani kuleta mabadiliko chanya katika jamii kupitia taasisi zao, jambo lililowasukuma kuanzisha mafunzo hayo ya uongozi ili kuwajengea uwezo wa kimfumo na kimkakati. "Tuliona kuna haja ya kuimarisha uwezo wa viongozi vijana kwa kuwapatia mbinu za kukabiliana na changamoto mbalimbali, kuboresha mifumo ya taasisi zao...
Comments
Post a Comment