Posts

Showing posts from April, 2024

BASATA YATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI

Image
  Naibu Katibu Mkuu Dkt. Suleman Serera ameagiza Baraza la Sanaa la Taifa kusimamia suala la maadili kuanzia ngazi ya msingi ili kuepuka madhara katika jamii na kizazi kijacho. Ameyasema hayo leo tarehe 24 Aprili, 2024 jijini Dar es salaam alipotembelea na kuongea na menejimenti ya Baraza huku akiweka wazi kuwa sanaa ina ushawishi mkubwa kuhamasisha jamii na kuijenga vile inavyotaka. Naibu Katibu Mkuu ameongeza kuwa, Baraza la sanaa lifuatilie kwa karibu na ufanisi juu ya namna bora ya kuimba wimbo wa Taifa na uzalendo kwa usahihi.

PARIMATCH BINGWA MSIMU WA TATU

Image
  MENEJA wa MasokoParimatch Lewis Paul amewataka Vijana kutumia mitandao ya kijamii Vizuri nakutotumia kwa mihemuko ilikepusha Madhara yanayoweza kutokea marabaada ya kutumia mitandao hiyo Ujumbe wa maudhui yasiyo na Maadili Mitandaoni. Akizungumza katika Uzinduzi wa Msimu Mpya wa Bingwa season 3 inayorurshwa na Chanel ya Startimes jijini Dar es salaam Lewis Paul amesema kuwa maudhui yanayotolewa na baadhi ya watoaji wa maudhui hayo kutoa maudhui hayo kwa uangalifu ilikuepusha madhara yatakayo patikana na matumiaji wa mitandao hiyo. "Ningependa kutoa ushauri kidogo kwa watu binafsi lazima ujiulize Msingi wa maudhui ,watuwengi huposti maudhui kwa mihemuko" Alisema Afisa Masoko Pari Match Lewis Paul Naye Mkurugenzi wa kwanza infinix Margreth Laurence amewataka Vijana kuweza kutumia mitandao ya kijamii nakusisitiza kuwa matumizi mabaya mitandao ya kijamii huleta Athari za kisakolojia kwa vijana. kwa Upande wake Muwakilishi wa Bodi ya  filamu nchini Boke Kilonzo amewataka Vijana ...

WASANII DIRISHA LA KUSAJILI KAZI ZA WASANII LIMEFUNGULIWA

Image
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dirisha la kupokea kazi za Sanaa limefunguliwa Leo  February 19  2024 na litafungwa Mei 9 Mei mwaka huu wasanii kusajili kazi zao zitakazowania tuzo za Tanzania Music Awards zinazotarajia kufanyika June 14 hadi 15 katika ukumbi wa The Super Dome uliopo Masaki jijini Dar es Salaam. Akizungumza Mwenyekiti wa kamati ya tuzo za Muziki Tanzania David Minja amewatangazia wasanii na waandaaji wa kazi za Sanaa nchini na Afrika kwa ujumla kwamba mfumo rasmi utakaotumika kuwakilisha kazi za muziki kwa hatua za uthaminishaji  kwenye kinyanganyiro cha tuzo za Muziki Tanzania kwa mwaka 2024. "Leo tarehe 19 mwezi April 2024, tumefungua rasmi mfumo wa upokeaji wa kazi za Sanaa na waandaaji wa kazi za Sanaa nchini umefunguliwa rasmi utakaotumika kuwakilisha kazi za Sanaa nchini kwa lengo la kuanza hatua za utathminishaji kwenye kinyanganyiro cha tuzo za Muziki Tanzania mwaka 2024." "Kiungo au link itakayotumika kuwasilisha kazi za muziki za shiriki ni t...

MSIMU WA TATU WA SHINDANO LA BINGWA KUZINDUALIWA

Image
Msimu wa tatu wa shindano la  bingwa umezinduliwa ambapo vijana 24 wenye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii wanatarajiwa kutafutwa ili  kuingia katika jumba maalum kuonesha uhalisia wa maisha yao. Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye uzinduzi wa shindano hilo  Meneja miradi wa Tv3 Ombeni Phiri alisema msimu huu kwa mara ya kwanza wataenda katika mikoa mitano ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam kuanzia mwezi ujao. "Msimu wa tatu wa bingwa umekuja kivingine kwanza tunaenda na mikoani lakini pia, tumepata mdhamini Pari match atakayeshirikiana na Startimes kutuunga mkono lengo ni kuwafikia vijana wengi,"alisema  Amesema mwaka huu watachukua washiriki 10 kila mkoa na baadaye watapigiwa kura ili kubaki 24 watakaoingia kwenye jumba kwa siku 70 na baadaye mshindi wa jumla kuondoka na zawadi yenye thamani ya sh milioni 35. Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui wa Startimes David Malisa alisema wao wameandaa zawadi mbalimbali ikiwemo posho za kila siku  kwa was...

WAZIRI KATAMBI AZINDUA MPANGO WA KUSAIDIA VIJANA UNFDPA

Image
Uzinduzi wa Awamu ya pili mpango wa Mradi Mpya wa Vijana wa UNFPA kwa Kushirikiana na Serikali, ambao umefanyika jijini Dar-es-Salaam. Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mradi huo Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Patrobas Katambi amesema kuwa  Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Idadi ya Watu (UNFPA) pamoja na Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzania kwa kunipa heshima ya kuhudhuria na kuzindua Programu ya “Safeguard Young People” Awamu ya Pili. "Ni furaha kubwa kwangu kushiriki katika uzinduzi huu muhimu ambao unalenga kuleta mabadiliko chanya kwa vijana wetu.Ninatambua na kuthamini juhudi kubwa zinazofanywa na UNFPA pamoja na Ubalozi wa Switzerland katika kusaidia juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha maisha ya vijana wetu. Programu hii ya “Safeguard Young People” ni muhimu sana katika kutoa msaada, elimu na fursa kwa vijana wetu ili waweze kujikwamua na changamoto wanazokabiliana nazo na kufikia mafan...

MILIONI 50 KUSHINDANIWA KATIKA KUANDIKA STORE OF CHANGE

Image
Baada ya mafanikio ya Shindano la Uandishi la 'Stories of Change' katika Mwaka 2021, 2022 na 2023, kwa mara nyingine JamiiForums inazindua Msimu mpya wa Shindano hilo kwa Mwaka 2024 kwa kushirikiana na Taasisi ya TWAWEZA. Akizungumza na waandishi wakati akifungua Msimu mpya, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo amesema Dhima ya Shindano la ‘Stories of Change’ (SoC) Mwaka 2024 ni “Tanzania Tuitakayo” ikilenga kuhamasisha Wananchi kuibua mawazo mbadala ya nini kifanyike kuipata Tanzania iliyobora zaidi kwa kupendekeza mawazo bunifu. Amefafanua kuwa Mawazo haya ni lazima yawe yale yanayoweza kutekelezeka ndani ya Miaka 5, 10, 15 hadi 25 ijayo na kuwa Shilingi Milioni 50 imetengwa kwa ajili ya washindi watakaoshiriki katika Shindano hilo linalotarajiwa kuanza Mei Mosi, 2024 hadi Juni 30, 2024. Misimu iliyopita ya Shindano la ‘Stories of Change’ (SoC), takribani machapisho 6,000 yaliwasilishwa ndani ya JamiiForums.com kutoka kwa Wananchi. Ameeleza kuwa Miongoni mwa Maudh...

WASHINDI 56 MTOKO WA KIBINGWA BETIKA JUKWAA LA VIP DERBY YA KARIAKOO DIMBA LA MKAPA KESHO

Image
  WASHINDI 56 Promosheni ya Mtoko wa Kibingwa msimu wa 07 kuitazama Derby ya Kariakoo kati Simba na Yanga itakayofanyika kesho kwenye uwanja wa Mkapa Jijini DaresSalaam. Akizungumza na Wanahabari mapema Leo Aprili 19,2024 Afisa Habari wa Kampuni ya Betika Tanzania Juvenalius Rugambwa wakati akiwapokea Washindi Promosheni ya Mtoko wa Kibingwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere amesema washindi hao wamepatikana kupitia droo ya mtoko Kibingwa iliyoanza Mapema Februari 2024. "Kama mnavyowaona hawa ni washindi ambao wamepatikana kupitia kampeni yetu ya mtoko kibingwa,na hawa washindi waliowasili Leo wataenda kuungana na wenzao wa Dar es Salaam nakukamilisha idadi kamili ya washindi 56 na wote watakwenda kulala kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tano wakifatiwa na bata la Mbagala zakiem kushuhudia burudani ya Muziki wa Bongofleva itakayodondoshwa na chino Wana Man,Mczo,platform, sholo Mwamba na wengine kibao." .Jevenalius ameongeza kuwa Msimu huu wa mtoko wa kib...