MSIMU WA TATU WA SHINDANO LA BINGWA KUZINDUALIWA



Msimu wa tatu wa shindano la  bingwa umezinduliwa ambapo vijana 24 wenye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii wanatarajiwa kutafutwa ili  kuingia katika jumba maalum kuonesha uhalisia wa maisha yao.

Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye uzinduzi wa shindano hilo 

Meneja miradi wa Tv3 Ombeni Phiri alisema msimu huu kwa mara ya kwanza wataenda katika mikoa mitano ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam kuanzia mwezi ujao.

"Msimu wa tatu wa bingwa umekuja kivingine kwanza tunaenda na mikoani lakini pia, tumepata mdhamini Pari match atakayeshirikiana na Startimes kutuunga mkono lengo ni kuwafikia vijana wengi,"alisema 

Amesema mwaka huu watachukua washiriki 10 kila mkoa na baadaye watapigiwa kura ili kubaki 24 watakaoingia kwenye jumba kwa siku 70 na baadaye mshindi wa jumla kuondoka na zawadi yenye thamani ya sh milioni 35.

Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui wa Startimes David Malisa alisema wao wameandaa zawadi mbalimbali ikiwemo posho za kila siku  kwa washiriki watakaokaa ndani ya jumba na kwa wale watakaopata umaarufu zaidi ndani ya jumba la bingwa.

Amesema atakayefanya vizuri msimu huu atachaguliwa pia,kuwa balozi wa Startimes.

Msimamizi wa vipindi wa Tv3 Emmanuel Sikawa alisema vijana watakaokuwa kwenye jumba hilo watapewa elimu ya maisha, namna ya kutumia fursa za kiuchumi, kuepuka matumizi ya dawa za kulevya na namna ya kutumia mitandao ya kijamii.

Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA