WASANII DIRISHA LA KUSAJILI KAZI ZA WASANII LIMEFUNGULIWA


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dirisha la kupokea kazi za Sanaa limefunguliwa Leo  February 19  2024 na litafungwa Mei 9 Mei mwaka huu wasanii kusajili kazi zao zitakazowania tuzo za Tanzania Music Awards zinazotarajia kufanyika June 14 hadi 15 katika ukumbi wa The Super Dome uliopo Masaki jijini Dar es Salaam.


Akizungumza Mwenyekiti wa kamati ya tuzo za Muziki Tanzania David Minja amewatangazia wasanii na waandaaji wa kazi za Sanaa nchini na Afrika kwa ujumla kwamba mfumo rasmi utakaotumika kuwakilisha kazi za muziki kwa hatua za uthaminishaji  kwenye kinyanganyiro cha tuzo za Muziki Tanzania kwa mwaka 2024.


"Leo tarehe 19 mwezi April 2024, tumefungua rasmi mfumo wa upokeaji wa kazi za Sanaa na waandaaji wa kazi za Sanaa nchini umefunguliwa rasmi utakaotumika kuwakilisha kazi za Sanaa nchini kwa lengo la kuanza hatua za utathminishaji kwenye kinyanganyiro cha tuzo za Muziki Tanzania mwaka 2024."


"Kiungo au link itakayotumika kuwasilisha kazi za muziki za shiriki ni tanzaniamusicawards.com Mlango wa kuwasilishaji wa kazi unafunguliwa 19 Aprili 2024 saa kumi alasiri na unafungwa mnamo 9 Mei 2024 saa tisa na dakika hamsini na tisa alasiri utakuwa mwisho wa ukusanyaji wa kazi za muziki."amesema Minja


Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BAraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Kedmon Mapana amesema wasanii watakao sajili kazi zao lazima wawe wamejisajili BASATA.

"Hakuna kazi ya muziki itakayoingia kwenye tuzo bila kupitia katika mfumo huo, wasanii wote wa kutoka Tanzania inabidi wawe wanachama hai wa BASATA kabla ya kuwasilisha kazi zao."amesema 

Naye Mirisho Mrisho kutoka Baraza la Sanaa la Taifa BASATA amesema kuwa zoezi hili linaanza Mei 9 litadumu kwa siku 21 kuwakilisha kazi za wasanii.

"Vipengele vilivyopo ni muziki wa dansi, hip hop, bongo fleva, Singeli na muziki wa asili, na Taarabu zote zimezingatiwa.

"Mwanamuziki Bora wa mwaka mwanamke na mwanaume,  Mwanamuziki wa dansi, mwanamuziki bora, dj, na waandaaji wa kazi za muziki."amesema Mrisho

Ameongeza kuwa Sharti kubwa msanii lazima awe amejisajili BASATA ilikuweza kuwania kinyanganyiro hicho cha tuzo za Muziki nchini.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA