WAZIRI KATAMBI AZINDUA MPANGO WA KUSAIDIA VIJANA UNFDPA
.png)
Uzinduzi wa Awamu ya pili mpango wa Mradi Mpya wa Vijana wa UNFPA kwa Kushirikiana na Serikali, ambao umefanyika jijini Dar-es-Salaam.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mradi huo Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Patrobas Katambi amesema kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Idadi ya Watu (UNFPA) pamoja na Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzania kwa kunipa heshima ya kuhudhuria na kuzindua Programu ya “Safeguard Young People” Awamu ya Pili.
"Ni furaha kubwa kwangu kushiriki katika uzinduzi huu muhimu ambao unalenga kuleta mabadiliko chanya kwa vijana wetu.Ninatambua na kuthamini juhudi kubwa zinazofanywa na UNFPA pamoja na Ubalozi wa Switzerland katika kusaidia juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha maisha ya vijana wetu. Programu hii ya “Safeguard Young People” ni muhimu sana katika kutoa msaada, elimu na fursa kwa vijana wetu ili waweze kujikwamua na changamoto wanazokabiliana nazo na kufikia mafanikio katika maisha yao.Ninapenda pia kutoa shukrani za pekee kwa timu nzima iliyohusika katika maandalizi ya uzinduzi huu. Bila juhudi zenu zenye bidii na uzalendo, tusingeweza kufanikisha tukio hili kwa mafanikio makubwa kama tuliyoyashuhudia leo.
Kwa upande wake Balozi kutoka Switzerland Tanzania H.E. Didier Chassot amesema hii inaleta chachu vijana kujisajili na kujikwamua kiuchumi katika kusaidia Taifa.
Naye UNFPA Representative Mark Bryan amesema kuwa vijana wanapoonyesha juhudi zao kutokana na bidii wanazoonyesha katika kutenda kazi kwa bidii.

Comments
Post a Comment