BASATA YATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI
Naibu Katibu Mkuu Dkt. Suleman Serera ameagiza Baraza la Sanaa la Taifa kusimamia suala la maadili kuanzia ngazi ya msingi ili kuepuka madhara katika jamii na kizazi kijacho.
Ameyasema hayo leo tarehe 24 Aprili, 2024 jijini Dar es salaam alipotembelea na kuongea na menejimenti ya Baraza huku akiweka wazi kuwa sanaa ina ushawishi mkubwa kuhamasisha jamii na kuijenga vile inavyotaka.
Naibu Katibu Mkuu ameongeza kuwa, Baraza la sanaa lifuatilie kwa karibu na ufanisi juu ya namna bora ya kuimba wimbo wa Taifa na uzalendo kwa usahihi.


Comments
Post a Comment