Posts

Showing posts from November, 2025

MSAMA: TUWAPUUZE WANAOLIPWA KUVURUGA AMANI YETU*

Image
Mfanyabiashara malufu nchi Tanzania Ndugu Alex Msama amewataka Watanzania kuwapuuza watu ambao wanalipwa ili kuvuruga amani ya nchi yetu ya Tanzania na mara nyingi sio Watanzania na baadhi yao ni Watanzania wanaoishi nje ya nchi kama vile Kenya na mataifa mengine ya nje. "Watanzania wenzangu, nawasihi kwa moyo mmoja tuwapuuze watu wanaotaka kuvuruga amani yetu, maana watu hawo wanalipwa Mamilioni ili kuvuruga amani yetu tuliyo nayo pia watu hawo hawaishi hata hapa nchini bali wanaishi nje ya nchi, wengi sio Watanzania na wanalipwa na baadhi ya Watanzania na watu wengine wa nje ya nchi ili wavuruge amani yetu iliyoasisiwa na wazee wetu , watu hawo furaha yawo nikuona amani yetu inavurugika ili watuibie Rasilimali zetu, pia furaha yao ni kuona tunagombana, tunauana na kuchukiana, tuwapuuze"

MSAMA ATOA WITO KWA WAZAZI, VIONGOZI WA DINI KUWALINDA VIJANA DHIDI YA VURUGU

Image
ALEX MSAMA WITO KWA WAZAZI, VIONGOZI WA DINI KUWALINDA VIJANA DHIDI YA VURUGU MKURUGENZI wa Msama Promotion, Alex Msama, ameetoa wito kwa wazazi nchini kukaa karibu na watoto wao na kuwashauri kuepuka ushawishi wa kujiingiza kwenye vitendo vya vurugu na misukumo isiyo na tija. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Msama alisema wazazi wana jukumu kubwa la kuhakikisha vijana wanalelewa katika misingi ya maadili na uzalendo, kwa kuwa wao ndio wamewazaa na kuwalea. “Mimi kama mzazi niseme kuwa watoto ni wetu, tumewazaa na kuwalea. Tuna uwezo wa kukaa nao, kuzungumza nao na kuwaonya. Tusikubali waingie kwenye mkumbo wa kufanya vurugu,” amesema Msama. Amesisitiza kuwa hakuna mtu mwenye mapenzi ya dhati kwa Tanzania zaidi ya Watanzania wenyewe, hivyo ni muhimu kuepuka kufuata mkumbo usio na manufaa kwa taifa. “Amani tuliyonayo ni ya muhimu sana. Tumeachiwa na waasisi wetu, wazazi na mababu zetu. Tunapaswa kuilinda kwa nguvu zetu zote,” ameongeza. Msama ...

OSMAN AAHIDI KUMCHAPA MAZOMBE

Image
Osama aahidi kum hapa Mazome mapema Na Brigitte Davis DAR ES SALAAM: BONDIA kutoka Mtwara, Osama Alabi, ambaye ameweka kambi yake ya maandalizi Mazense ametangaza kumkalisha mpinzani wake Ally Mazome wa Morogoro kwa TKO katika pambano la Boxing on Boxing Day litakalofanyika Desemba 26, 2025 katika Ukumbi wa Warehouse, Masaki. Akizungumza m Dar es Salaam , Alabi anayefahamika pia kama Osama Korosho amesema amejipanga vizuri kuhakikisha anapata ushindi katika pambano hilo akisisitiza kuwa mashabiki wa Mtwara na Watanzania kwa ujumla wawe sehemu ya “historia mpya” ambayo anatarajia kuiandika ulingoni. “Nimejiandaa vya kutosha, naimani hii ndiyo siku yangu. Naomba mashabiki wangu wote wa Mtwara na Watanzania waje kushuhudia ushindi wa kihistoria,”alisema. Kwa upande wa mashabiki wake, wameeleza kujiamini kuwa Osama ataibuka na ushindi mnono wakifananisha uwezo wake na “paka aliyekula mboga ya familia.” “Tumejiandaa, Osama anashinda bila shaka,” — Eliud Mwakapala (Shabiki) “Siku ...

DAR CITY WARUDI WAKIWA WAMESHINDA NAFASI YA 3

Image
Nahodha wa Dar City: “Mchezo Ulikuwa Mgumu, Lakini Tumepambana Mpaka Mwisho” NAHODHA wa Timu ya Basketball ya Dar City, HasheemThabit, amesema mashindano waliyoshiriki nchini Kenya yalikuwa na ushindani mkubwa, lakini wanashukuru kwa nafasi waliyoipata na matokeo waliyofikia. Akizungumza mara baada ya kurejea nchini, Thabiti amesema mchezo wa basketball una siku zake, na si kila mara matokeo huwa upande mmoja. “Basketball ni mchezo wa tofauti; si kila siku mchezo utakuwa wako. Kuna siku utaongoza, na kuna siku utapata changamoto. Wachezaji gani tunawahitaji, tunaweza kuendelea nao, na wapi wanauwezo mdogo hayo yote tunapaswa kuyapima,” amesema Thabiti. Nahodha huyo ameendelea kusisitiza kuwa ameshinda michezo mingi ya basketball na anaifahamu vema namna mchezo unavyobadilika kulingana na mazingira na ubora wa timu pinzani. Klabu ya Dar City ilishukuru Mungu kwa mafanikio waliyoyapata katika mashindano hayo, ikiwemo kushika nafasi ya tatu, ikiwa ni ishara ya uwakilishi m...

DAR CITY WAMEFUZU HATUA BAADA YA USHINDI VIKAPU 92 KWA 77

Image
Timu ya mpira wa Kikapu ya Dar City leo imeandika historia mpya baada ya kufanikiwa kuwa timu ya kwanza ya Tanzania kufuzu kucheza fainali za BAL 2026 (Basketball African League). Dar City wamefuzu hatua hiyo baada ya ushindi wa vikapu 92-77 dhidi ya Club Ferroviario ya Msumbiji, Dar City wamemaliza nafasi ya tatu katika hatua ya Elite 16.

DAR CITY YAFIKA NUSU FAINALI AFRIKA

Image
KLABU ya Dar City imeweka historia mpya baada ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kufuzu Fainali za Ligi ya Afrika, kufuatia rekodi ya ushindi katika michezo yake yote mitatu ya Kundi B. Katika mchezo wa kwanza, Dar City ilianza kwa kishindo baada ya kuichapa Matera Magic kwa pointi 85–78, kabla ya kuendeleza ubabe kwa kuilaza Brave Hearts kwa 93–75. Timu hiyo kutoka Tanzania ilikamilisha hatua ya makundi kwa ushindi mwingine muhimu dhidi ya Ferroviario kwa 87–78, na kujihakikishia nafasi kileleni mwa kundi. Kutokana na matokeo hayo, Dar City sasa inasubiri kukutana na timu itakayomaliza katika nafasi ya pili kwenye Kundi B, pambano litakalokuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora uliooneshwa na kikosi hicho tangu mwanzo wa mashindano. Dar City iwapo itafanya vizuri katika hatua hiyo ya nusu fainali basi itakuwa ni miongoni mwa timu tatu zitakazowakilisha kwenye fainali za ligi ya kikapu Afrika zitakazofanyika Kigali, nchini Rwanda mwakani.

STEVE NYERERE NA ASASI WAKABIDHI MILION TANO MSIBA WA MC PILIPILI.

Image
MWENYEKITI wa Taasisi ya Mama Ongea Na Mwanao Steve Mengele iSteve Nyererei amesema Pilipili ameondoka kipindi ambacho taifa linamuhitaji. Akizungumza wakati wa Salamu za Pole Kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Marehemu MC PiliPili Nchi Nzima inamlilia. Aidha kama Mama Ongea na Mwanae wametoa kiasi cha Sh Milioni tano kitaka endakusaidia elimu kwa watoto wa marehemu Mc Pilipili. Steve Nyerere Ameeleza Kuumizwa Sana na Kifo Cha Mc PiliPili Ikiwa Kama Nchi Imempoteza Mtu mahiri Sana. "PiliPili ameondoka muda ambao kama nchi ilikuwa inamuhitaji kuongeza nguvu kazi"amesema Marehemu MC PiliPili Amezikwa Leo Jioni Huko Jijini Dodoma,Tanzania.

NICE TO MEET YOU MSIMU WA PILI HUKU LIPA TUKUBUSTI

Image
“‘Nice to Meet You’ Yazindua msimu wa pili, wasanii watakiwa kuongeza viwango kuboresha filamu za Tanzania” TAMTHILIA maarufu Nice to Meet You imemtambulisha rasmi msanii mpya, Tasu, katika uzinduzi wa msimu wake wa pili, huku wadau wa filamu nchini wakihimiza utengenezaji wa kazi zenye ubora na viwango vya kimataifa ili kukuza hadhi ya soko la filamu Tanzania na kuinua vipaji vipya. Akizungumza katika uzinduzi huo, Munirah Pendeza, 'Tusa' ndani ya tamthilia hiyo, amesema sekta ya filamu kwa sasa imekuwa na hamasa, morali na motisha kubwa miongoni mwa watayarishaji, hivyo wasanii wanapaswa kufanya kazi kwa ubora zaidi ili kuendana na kasi hiyo. Tusa amewahimiza mashabiki kutumia ofa maalumu ya msimu wa sikukuu kwa kulipia ving’amuzi vya StarTimes, ili kufurahia maudhui mbalimbali ikiwemo tamthilia ya Nice to Meet You, katuni za watoto kama Bonnie Bears (maarufu kama Kipara Mbabe), Super Wings, pamoja na maudhui ya michezo na tamthilia zilizotafsiriwa kwa Kiswahili. Kwa up...

JK AONGOZA MAHAFALI YA 55 (DURU LA PILI) YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM UKUMBI WA MLIMANI CITY JIJINI DAR

Image
UDSM yamtunuku Dkt. Maria Kamm Shahada ya Heshima kutokana na mchango wake katika elimu nchini DAR ES SALAAM MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ametunuku Shahada za Awali, Stashahada na Astashahada kwa wahitimu katika Mahafali ya 55 (Duru la Pili) ya chuo hicho kikongwe kuliko vyote nchini. Jumla ya wahitimu 2,742 walihudhurishwa kwenye mahafali hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. katika hatua nyingine Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimemtunuku Digrii ya Heshima ya Udaktari wa Fasihi Mwasisi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Clementina, Dkt. Maria Josephine Kamm, kutokana na mchango wake mkubwa na wa muda mrefu katika kuendeleza elimu nchini. Tuzo hiyo imetolewa leo, Novemba 18, 2025, wakati wa mahafali ya 55 ya UDSM yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, yakihudhuriwa na maelfu ya wahitimu, wazazi na wageni waalikwa. Akizungumza baada ya kutunukiwa, Dkt. ...

STEVE NYERERE: DARAJA LA JAMII NA MWANAHARAKATI WA MAENDELEO

Image
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steven Waiton Mengele, maarufu kama Steve Nyerere, ni miongoni mwa wadau muhimu wa maendeleo nchini kupitia mchango wake mkubwa katika sanaa za maigizo na uchekeshaji kwa miaka mingi. Kwa muda mrefu, Steve ameendelea kuwa nguzo kwa makundi mbalimbali yenye uhitaji, wasanii na wadau wa sanaa kwa ujumla, akihakikisha anakuwa daraja la kusaidia na kuunganisha watu wanaohitaji msaada kwa namna moja au nyingine. Kupitia jitihada zake binafsi pamoja na ushirikiano kutoka kwa wadau wa ndani na nje ya nchi, amefanikiwa kupunguza au kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watu aliofikiwa. Rekodi zinaonesha kuwa Steve amekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha upatikanaji wa misaada ya hali na mali kwa watu wengi, hususan pale ambapo jambo liko ndani ya uwezo wake kulishughulikia. Nia yake thabiti ya kuleta mabadiliko chanya imeendelea kumjengea uaminifu mkubwa kutoka kwa taasisi, viongozi, wadau na jamii, kiasi cha kutazamwa kama da...

AFRICA KUKUTANA ARUSHA MKUTANO WA TEKNOLOJIA YA AKILI MNEMBA (APAIC 2025) NOVEMBA 24 HADI 27

Image
Washiriki zaidi ya 1,200 kutoka nchi zaidi ya 40 wanatarajiwa kushiriki Mkutano wa Kilele wa Akili Unde Afrika (APAIC 2025) utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Novemba 24 hadi 27, 2025, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Mkutano huo unatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kimataifa litakalojadili matumizi ya teknolojia ya Akili Mnemba (Unde) katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, kilimo, biashara na utawala bora. Akizungumza kuhusu maandalizi ya mkutano huo, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa APAIC 2025, Abdulwahid Ali Khamis, alisema tukio hilo litaweka historia mpya katika safari ya mageuzi ya kidijitali barani Afrika, likilenga kuunganisha serikali, sekta binafsi, wawekezaji, taasisi za elimu na wabunifu wa teknolojia. “Afrika ipo katika kipindi muhimu cha kuamua njia ya mageuzi yake ya kijamii na kiuchumi kupitia akili unde. Huu ni wakati wa kuweka misingi ya matumizi jumuishi, bunifu na yenye maadili ya teknolojia hiyo,” amesema Khamis. Amee...

AFRICA KUKUTANA ARUSHA MKUTANO WA TEKNOLOJIA YA AKILI MNEMBA (APAIC 2025) NOVEMBA 24 HADI 27

Image
Washiriki 1,200 kuhudhuria mkutano wa teknolojia ya Akili Unde Afrika (APAIC 2025) Arusha Washiriki zaidi ya 1,200 kutoka nchi zaidi ya 40 wanatarajiwa kushiriki Mkutano wa Kilele wa Akili Unde Afrika (APAIC 2025) utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Novemba 24 hadi 27, 2025, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Mkutano huo unatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kimataifa litakalojadili matumizi ya teknolojia ya Akili Mnemba (Unde) katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, kilimo, biashara na utawala bora. Akizungumza kuhusu maandalizi ya mkutano huo, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa APAIC 2025, Abdulwahid Ali Khamis, alisema tukio hilo litaweka historia mpya katika safari ya mageuzi ya kidijitali barani Afrika, likilenga kuunganisha serikali, sekta binafsi, wawekezaji, taasisi za elimu na wabunifu wa teknolojia. “Afrika ipo katika kipindi muhimu cha kuamua njia ya mageuzi yake ya kijamii na kiuchumi kupitia akili unde. Huu ni wakati wa kuweka misingi...

'C' EST JESUS YA NANA MARIAM KUTOKA NOVEMBA 16

Image
"" border="0" data-original-height="990" data-original-width="1080" src="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgKsipYh0XJCvlJw7d2FgyJDUJhyphenhyphenKEht5drJIVgrZMcTZBke_hygHYH_u23_OZFnccxwC9cwF_EKT3yQn1-oTHXJHkfcFHRwrFB6dmteP8zMgGqiXOZSw6QJp9H-393PpvCKGGsjqaKbVjKv42a5p817SDKrW-m940X58mtvcKvT4igm-tQhcq5Hthv_Mfn/s1600/Screenshot_20251111-135419.png"/> 'C'est Jesus' ya Nana Miriam kutoka Novemba 16 MWIMBAJI anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Injili nchini Kongo, Nana Miriam ameachia kionjo cha wimbo mpya, C'est Jésus, alioshirikiana na Sylvain Kashila. Waimbaji hao ambao kwasasa ni tishio nchini Kongo, wameteka hisia za mashabiki wa muziki huo punde baada ga kuachia kionjo cha ngoma hiyo inayotarajia kutoka Novemba 16, mwaka huu. Akizungumzia kolabo hiyo Nana Miriam, amewataka mashabiki wa Afrika Mashariki na Kati wakae mkao wa kumtukuza Mungu kupitia wimbo huo uliowabariki wengi. "...

ARUSHA MWENYEJI MKUTANO WA AKILI MNEMBA AFRIKA

Image
Arusha Yashika Hatamu – Mkutano wa Kwanza wa Afrika wa Akili Mnemba (AI) Kufanyika Novemba 2025 JIJI la Arusha linajiandaa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Afrika wa Akili Mnemba (Africa Premier AI Conference – APAIC 2025) utakaofanyika kuanzia Novemba 24 hadi 27, 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa APAIC 2025, Abdulwahid Ali Khamis, mkutano huo utalenga kujadili na kuweka mikakati ya maendeleo ya Akili Mnemba (AI) barani Afrika, chini ya kauli mbiu “Kuchambua Agentic AI kwa Mageuzi ya Kijamii na Kiuchumi Barani Afrika.” "Zaidi ya wajumbe 1,200, wazungumzaji 150, na washiriki kutoka zaidi ya nchi 40 wanatarajiwa kuhudhuria. Tofauti na makongamano mengine, APAIC 2025 italenga zaidi utekelezaji wa ubia kati ya serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wabunifu ili kutumia AI kuboresha afya, elimu, kilimo, biashara na utawala bora. "Mkutano huo unaandaliwa kwa ushirikiano wa ScanCode Tanzania,...

UVCCM YAKEMEA VURUGU ZA OKTOBA, AMANI NI MSINGI WA MAENDELEO

Image
UVCCM Yakemea Vurugu za Oktoba, Yasema Amani ni Msingi wa Maendeleo DAR ES SALAAM:MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) amelaani na kuvunja ukimya, kwa masikitiko makubwa kuhusu matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea Oktoba 29 na 30, 2025, ambayo amesema kwa kiasi kikubwa yalihusisha vijana. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari, Mwenyekiti wa (UVCCM) Mohamed Kawaida amesema kuwa matukio hayo yameacha majeraha makubwa katika jamii, hasa ikizingatiwa kuwa yalifanywa na kundi la watu ambalo yeye mwenyewe ana dhamana ya kuwaongoza ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). “Leo nimesimama mbele yenu si kwa furaha, bali kwa huzuni kubwa moyoni mwangu. Uchaguzi uliopita ulioleta matokeo mazuri kwa chama chetu, umeambatana na vurugu na fujo ambazo zimeacha alama za maumivu na hasara kubwa kwa taifa,” amesema . Ameongeza kuwa kitendo cha vijana kushiriki katika vitendo vya vurugu ni kinyume cha maadili, sheria na utaratibu wa kijamii, huku...