ARUSHA MWENYEJI MKUTANO WA AKILI MNEMBA AFRIKA

Arusha Yashika Hatamu – Mkutano wa Kwanza wa Afrika wa Akili Mnemba (AI) Kufanyika Novemba 2025
JIJI la Arusha linajiandaa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Afrika wa Akili Mnemba (Africa Premier AI Conference – APAIC 2025) utakaofanyika kuanzia Novemba 24 hadi 27, 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa APAIC 2025, Abdulwahid Ali Khamis, mkutano huo utalenga kujadili na kuweka mikakati ya maendeleo ya Akili Mnemba (AI) barani Afrika, chini ya kauli mbiu “Kuchambua Agentic AI kwa Mageuzi ya Kijamii na Kiuchumi Barani Afrika.” "Zaidi ya wajumbe 1,200, wazungumzaji 150, na washiriki kutoka zaidi ya nchi 40 wanatarajiwa kuhudhuria. Tofauti na makongamano mengine, APAIC 2025 italenga zaidi utekelezaji wa ubia kati ya serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wabunifu ili kutumia AI kuboresha afya, elimu, kilimo, biashara na utawala bora. "Mkutano huo unaandaliwa kwa ushirikiano wa ScanCode Tanzania, HAM International, na kampuni ya kimataifa MindHYVE.ai ya Marekani, pamoja na washirika kama Wizara ya Elimu,COSTECH. "Miongoni mwa matukio muhimu ni uzinduzi wa The Dawn Directive – mfumo wa kwanza wa uelewa na umahiri wa AI duniani, pamoja na Azimio la Mombasa kuhusu Agentic AI litakaloweka dira ya Afrika kuhusu maadili na usimamizi wa teknolojia hiyo."amesema Khamis Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mkutano, Anthony Nivo, amesema kuchaguliwa kwa Arusha kuandaa APAIC 2025 ni uthibitisho wa nafasi ya Afrika Mashariki katika mapinduzi ya kidijitali. “AI si teknolojia ya kesho — ni ya leo,” amesema Nivo. “Kuandaa APAIC 2025 hapa Arusha ni hatua ya kihistoria katika kuamua jinsi Afrika itakavyonufaika na mapinduzi ya akili mnemba.”amesema Nivo

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA