STARTIMES ZOTE NDANI KAZI KWENU MASHABIKI
KAMPUNI ya Startimes imesema itaendelea kuunga mkono Ligi ya Championship ili kuwapa nafasi vijana kuonesha vipaji na kujiuza kimataifa. Imesema inatarajia kuonesha Ligi kubwa za Ulaya zikiwemo La Liga ya Hispania, Ujerumani Bundesliga, Saudi Arabia, Carabao Cup na Copa Del Rey. Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui kutoka Startimes David Malisa kwenye uzinduzi wa kampeni mpya ya zote ndani. “Ligi zote kubwa zitakuwa Startimes, tunaanza nyumbani na Championship kisha kimataifa na hiyo yote tunataka mashabiki zetu waendelee kubaki na sisi kwa kulipia vifurushi kwa bei ndogo na kuona namna vijana mbalimbali wanavyofanya vizuri,”amesema. Meneja vipindi na Maudhui kutoka Tv3 Emmanuel Sikawa amesema michuano hiyo yote itaruka kupitia Tv3 na kuhimiza mashabiki wa soka na wadau mbalimbali kutobaki nyuma bali ni wakati sahihi kuona vipaji vya soka vya ndani na kimatifa. Amesema wamekuwa wakifanya vizuri kuonesha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa migu...