NANDY NDIO ALINIAMBIA NIVAE KITOVU NJE
Msanii wa Bongo fleva nchini Yammy amesema kuwa anapovaa na kuacha kitovu wazi alishauriwa na Boss wake Faustina Mfinanga 'Nandy'
Yammy amesema kuwa awali alikuwa anashindwa kuvaa hivyo lakini siku zilivyozidi kwenda amejikuta amezoea.
"Watu wasichokijua Boss wangu Nandy ndie aliyenishauri kuvaa hivyo na kuacha kitovu nje kwa sababu nina umbo zuri na bado umri wangu ni mdogo hivyo nikivaa napendeza."
"Nandy hawezi kuvaa hivyo kwa sababu umri wake na wangu ni tofauti na ukizingatia yeye ameshakuwa mama anamtoto na ameolewa lakini kipindi cha nyuma akiwa na umri kama wangu ameshavaa sana."amesema Yammy
Pia Yammy ameweza kujizolea umaarufu zaidi tangu alipoanza kuvaa na kuacha kitovu nje hivyo ni sehemu ya kutembea na upepo huo anapotangaza kazi zake.
Lakini pia msanii kama Ray C, Rachel Kizunguzungu pamoja na Mwanadada Judith Wambura Lady Jay Dee ni miongoni mwa wasanii walipokuwa wakiacha vitovu nje lakini umri ulivyosogea waliacha.

Comments
Post a Comment