DSTV TUMEKUELEWA WASHUSHA VINGAMUZI
Kampuni ya MultiChoice Tanzania DStv imesema itaanza kuonesha tamthilia za kigeni kwa Lugha ya Kiswahili kuanzia Julai 20 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Masoko wa DStv Tanzania Baraka Shelukindo amesema sababu kubwa ya kuzitafsiri kwa Lugha ya Kiswahili ni kuhakikisha inawafikia Mamilioni ya wateja wake ukanda wa Afrika Mashabiki.
"Kupitia kampeni mpya ya Tumekusikiliza tunataka kuwafikia wateja wetu kwa burudani mbalimbali na sasa tunakuja na tamthilia za Kituruki kwa Lugha ya Kiswahili cha kufanya kwa wateja wetu ni kulipia vifurushi,"amesema.
Amesema "kila mtu hivi sasa lazima awe wa kimataifa kwa kumiliki DStv kirahisi na kuona mambo yote kama Mpira, Filamu na tamthilia mbalimbali,"amesema Shelukindo
Pia amesema kuwa 29 Julai kuanza itaanza kuruka tamthilia ya kigeni inayoitwa The Boy pia kutakuwa na thamthilia ya Kiswahili inayoitwa Yolanda itaanza kuruka rasmi katika Magic Bongo.


Comments
Post a Comment