TMDA :HAKUNA KIRUSI KINACHOKAA KWENYE DAWA HII



MAMLAKA ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) imekanusha kwa mara nyingine kuwa  hakuna virusi vinavyojulikana kwa jina la Machupo au  virusi vya aina yoyote haviwezi kuishi kwenye kidonge. 

Awali taarifa ilisambaa katika mitandao ya kijamii ikisema dawa aina ya Paracetamol ambayo imeandikwa P 500 na 

kudaiwa kubabua ngozi

Taarifa hiyo ilisema "Dawa hiyo inadaiwa kuwa ni ‘’paracetamol mpya nyeupe sana na inayong'aa,madaktari 

wanashauri kuwa ina virusi vya "Machupo", inayochukuliwa kuwa moja ya virusi 

hatari zaidi ulimwenguni, na kiwango cha juu cha vifo.

Aidha, Mtoa taarifa anaitaka jamii kuisambaza taarifa hii kwa kila mtu aliyeko katika orodha yake ya mawasiliano ili kuokoa maisha. ‘’Nimefanya 

sehemu yangu, sasa ni zamu yako. Kumbuka kwamba Mungu huwasaidia wale wanaosaidia wengine. ‘’Sambaza kama ilivyopokelewa,"amesema mtoa taarifa huyo 

Akitoa ufafanuzi kuhusu dawa hiyo katika taarifa yake Mkurugenziwa TMDA ,Adam Fimbo ameeleza kuwa, Taarifa hiyo imekuwa ikijirudia mara kwa mara na TMDA imekuwa ikitolea ufafanuzi

ikiwemo taarifa ya mnamo tarehe 10 Mei, 2023, juu ya dawa aina ya P-500® 

(PARACETAMOL) ya Apex Laboratories Private Limited, Tamil Nadu, India 

iliyodaiwa kuwa na virusi hivyo.

Amesema TMDA inapenda kuwahakishia wananchi kuwa inaendelea kutimiza wajibu wake wa 

kulinda afya ya Jamii kwa kuhakikisha kuwa bidhaa tiba zinazotumika nchini ni zile 

zenye kukidhi matakwa ya ubora, usalama na ufanisi.

Vilevile, Mamlaka inapenda kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kupata ufafanuzi 

kutoka kwenye mamlaka husika kabla ya kusambaza taarifa zinazoweza kuleta 

taharuki kwenye Jamii.

Aidha, Wananchi wanaweza kupiga simu ya bila malipo: 0800110084 endapo wapatapo taarifa za mashaka kama hizo.


Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA