DM MALL NA MMG WASHUSHA MIZOGO USHINGWE WEWE
Viwanda 25 vya China vimetua nchini kushiriki maonesho ya Sabasaba 2024 chini ya uratibu wa Kampuni za usafitishaji mizigo za Kitanzania za DM Mall na MMG Logistics.
Akizungumza na habari leo Mkurugenzi wa kampuni hizo Hamid Idrissa Hamid alisema lengo la ujio wa kampuni hizo ni kuonesha bidhaa wanazozalisha, kutengeneza mtandao na wafanyabiashara wa Tanzania lakini pia, kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuwavuta wawekezaji kutembelea nchini na kuona fursa zilizopo.
Ametaja miongoni mwa viwanda vilivyokuja ni pamoja na vya nguo, vifaa vya majumbani, simu, solar, viatu, mitambo, vinywaji, Jenereta, magari, vyakula, bidhaa za urembo na bidhaa mbalimbali ambapo pia, watatumia maonesho hayo kuuza na kuonesha shughuli zao.
"Lengo la kuwaleta hatutaki kikundi Cha watu kinufaike peke yao bali tunataka Mtanzania mmoja mmoja anufaike apate kitu kwa bei ndogo ili kuyavutia makampuni hayo kuwekeza nchini na hatimaye kufungua viwanda na kutoa ajira nyingi kwa vijana,"amesema.
Meneja Masoko wa DM Mall na MMG Logistics Haruna Said amesema baada ya kuona changamoto wanazopitia Wafanyabiashara wa Kitanzania, vijana wa Kitanzania waliosoma China waliona kuna haja ya kuwasaidia wafanyabiashara kwa kuwaunganisha na makampuni ya China kufanya biashara na kupata mizigo yao kwa wakati.
Alisema tangu wameanza ushirikiano na makampuni mbalimbali ya Kichina kwa ajili ya kufanya biashara na wafanyabiashara wa Tanzania kwa zaidi ya miaka mitano wameajiri vijana zaidi ya 35 hapa nchini na China sambamba na Wachina nane.
"Natoa wito kwa Watanzania waone fursa kupitia makampuni haya, tuna ushirikiano mzuri, bidhaa zao ni bei poa wakija na kutaka kufanya kazi na sisi watanufaika na nchi itaendelea kupata mapato kwa ajili ya kufanya maendeleo ya nchi, waje hapa Sabasaba kwenye Banda la Kichina waone bei za bidhaa kuanzia sh 100 kwa bei ya promosheni,"amesema.
Amesema ujio wa wafanyabiashara hao ni kutaka kuonesha umakini kwa kutangaza bidhaa zao original zenye Quality zikitoka katika miji tofauti ya China.
Pia ameongeza kuwa wanatoa wito kwa wafanya biashara wanaotaka kusafilishiwa biAa zao kupitia kampuni hiyo ili kuwasaidia kufikisha kwa wakati.
"Imezoeleka mtu anapoagiza mzigo wake kutoka china hufika Tanzania kwa kuchelewa lakini kampuni zetu ni za huhakika katika kufikisha bizaa kwa wakati na kufuatana na matumio kama siku za sikukuu.
"Sabasaba tutakuwa na zawadi tofauti tofauti kwa bei za kawaida ikiwa ni sehemu ya kutangaza bidhaa zetu hali itakayosaidia kupata vitu vyenye ubora.
Miongoni mwa wafanyabiashara kutoka Kampuni ya XY Cargo Feler Logistics ya China Xu Jian alisema wamechagua kuja Tanzania kwa kuwa ni sehemu salama kwa kufanya biashara lakini pia, wakitegemea kupata wateja wengi wa kushirikiana nao.
Wawakilishi wa viwanda hivyo wanatarajia kukutana hivi karibuni na wafanyabiashara wa Tanzania kubadilishana ujuzi ambapo Mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa Mipango na uwekezaji Professa Kitila Mkumbo.





Comments
Post a Comment