SHILOLE MUUZA CHAKULA ESHA NI MPISHI
Msanii wa Filamu nchini Esha Buheti ameweka bayana kuwa Zuwena Mohammed 'Shilole' ni muuza Chakula lakini yeye ni mapishi.
Esha Buheti amesema kuwa Shilole anaivisha chakula ili watu wale lakini yeye ni mpishi anayepika chakula kikaiva na watu Wakala.
"Mimi situmii karanga acha yeye aweke karanga kwenye tembele wali karanga kila chakula, kwa kupika Shilole hanipati hata kidogo, aache kuivisha chakula ajifunze upishi apike chakula kinachoeleweka.
"Lisemwalo lipo kama halipo laja akubali tu kwenye upishi hayupo ila, hii imekuja kutokana na kwenye ubaya wema ulikuwepo, ni kawaida sana rafiki kuwa adui ni rahisi kuliko adui kuwa rafiki."
Esha amesema "acha watu wamjaze wee na yeye anajaa nafutahia tu anachofanya sina muda wa kugombana yeye anapenda kidogo tupigane me napenda amani Shilole acha roho mbaya."
Aidha amesema kuwa "Zuwena ameshazoea kupiga wanaume siwezi kupigana aende akapigane na mwiliwake huko apungue asiwaze kupigana na Esha akishidwa aweke kiputo."amesema Esha
Hayo yametokana na maneno yanayoendele kwenye mitandao ya kijamii baina Esha na Zuwena Mohammed 'Shilole' nani mkali wa katika kupika.
Kwa upande wake Babalevo amesema kuwa Esha ni mpishi lakini Shilole ni mfanyabiashara anaijua.

Comments
Post a Comment