SNURA AIKIMBIA TASNIA YA SANAA
Snura amesema kuwa anajutia maisha haliyoyaishi akiwa msanii yaliokuwa mabaya yasiyompendeza Mwenyezi Mungu atamani hata kuwa mfano kwa mtu yoyote.
"Mimi Snura Mushi kuanzia leo nikiwa na akiri yangu timamu natangaza kuacha muziki na kazi zote zinazo husiana na sanaa nisihusishwe.
"Nimejitambua mimi ni mtoto wa kiislamu nimeamua kufanya yanayo mpendeza Mungu ibada na kumtumikia, niliamua kumrudia Mungu tangu miaka miwili iliyopita ndo mana uliona nipo kimya sijafanya chochote kinachohusiana na Sanaa."amesema Snura
Snura amesema kuwa anaomba asihusishwe wala kupigiwa simu kuhusu kitu chochote kinacho husiana na sanaa wala hana mpango navyo tena.
"Sitaki watu wapige nyimbo zangu zote na ikitokea siku nimefariki watu wasipost picha zangu za hovyo nilizowahi kupiga kwani najuta kwa kupiga picha hizo na sitaki watu wengine waige mfano wangu."
"Sitaki watu wapige nyimbo zangu zote na ikitokea siku nimefariki watu wasipost picha zangu za hovyo nilizowahi kupiga kwani najuta kwa kupiga picha hizo na sitaki watu wengine waige mfano wangu."
"Nimefanya mambo mengi mabaya yakumchukiza Mungu kitu ambacho sitamani hata mtu yoyote akumbuke wala kunikumbusha najuta sana kwanini tangu kipindi kile nisinge mrudia Mungu."amesema Snura

Comments
Post a Comment