HARMONIZE APATA DILI LA BUKUA MILIONI
Msanii wa Bongo fleva nchini Rajab Abdul 'Harmonize' amepata Dili la Mchezo wa kubashiri unaojulikana kama Bukua Mamilioni.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa Mchezo huo Harmonize amesema kuwa hii itasaidia watanzania kujishindia vitu mbali mbali.
"Ninafasi ya watanzania kujipatia ajira kupitia kampuni hii kwa kutumia pikipiki ambazo zitakuwa zikutolewa kila Ijumaa kwa mshindi atakaye shinda.
"Lakini zawadi hizo hazitakuwa kwa washindi wa Dar tu peke yao tutatoa hata kwa watakaoshinda mikoani nitahakikisha nawakabizi mwenyewe kwa mikono yangu zawadi yoyote atakayoshinda mshindi Mkoa wowote hule."amesema Harmonize


Comments
Post a Comment