GRAND GALA DANCE KUFANYIKA AGOSTI 30 THE SUPER DOME

 


Msimu wa tatu wa Grand Gala Dance kufanyika unatarajia kufanyika 30 Agosti 2024 katika ukumbi wa The Super Dome Masaki uliopo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Mkurugenzi wa Chocolate Princess na Muandaaji Mboni Masimba amesema kuwa Grand Gala Dance itapambwa na burudani kutoka kwa Bendi nne ikiwemo FM Academia.


"Usiku wa Grand Gala Dance imeanzishwa nahususi kwa ajili ya kumuhenzi Rais wa Awamu ya kwanza wa Jamhuri wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere na utakuwa na burudani kutoka kwa Bendi ya  FM Academia, Christian Bella, Twanga Peteta na Tukuyu Sound.


"Zitakazo konga nyoyo za watanzania  zitatumbuiza mubashara ikiwa ni kumbukizi ya kumuhenzi Baba wa Taifa kwa makubwa aliyoyafanya katika Taifa letu la Tanzania.


Naye Pancho Mwamba amesema kuwa wananchi watarajie muziki mzuri kutoka kwa Bendi ya AF Academia kumbuka sio mashindano Bali ni muziki mzuri kutoka kwao.

Kwa upande wake Christian Bella amesema kuwa hadi tarehe 30 atakuwa tayari ameachia albamu yake ya Rhumba hivyo watanzania watarajie mazuri kutoka kwa Malaika Bendi anayosimamia Bella.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA