TUSIWACHUKULIE POA MABEKI TATU
Msanii wa Filamu nchini Jacqueline Wolper amewaomba wanawake kuwapenda wadada wanao wasaidia kazi na kulea watoto wao nyumbani.
Jacqueline amesema wadada wa kazi nao wanauwezo mzuri na ushauri katika mambo mbalimbali, kama wazo lake la kujenga nyumba lilitoka kwa dada yake wake wa kazi
"Mimi wazo la kujenga nyumba nililipata kwa dada wa kazi (house girl) wangu, nilikuwa namlipa mshahara kumbe alikuwa anatunza hadi siku aliyokuja kuniambia anashukuru kwa pesa nizokukuwa nikimlipa.
"Dada nashukuru kwa msaada wako mimi nimejenga nyumba kupitia mshahara wako" Hapo ndipo akili ikanijia kuwa kumbe hata mimi naweza kujenga nyumba kwa kusevu pesa kidogo kidogo"
"Tangu hapo nilianza kusevu pesa kwa ajili ya nyumba na hatimae nikafanikiwa kujenga nyumba kubwa, nzuri ambayo thamani yake huenda ni zaidi ya shilingi milioni 500 za Tanzania ingawa bado haijaisha vizuri."
Pia Jacquline amesema kuwa anamshukuru house girl wake kwa kumpa wazo nzuri.

Comments
Post a Comment