RIBA YA BANKI KUU BADO ASILIMIA 6
Kamati ya Sera ya Fedha (MPC)ya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BOT) imeamua Riba ya Benki Kuu (CBR) itaendelea kuwa asilimia 6 kwa robo mwaka unaoishia Septemba 2024.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Naibu Gavana Kayanda Kayandabila amesema Uamuzi huu umefikiwa katika kikao cha Kamati kilichofanyika Julai 3,2024.
"Tathmini ya Kamati kuhusu mwelekeo wa uchumi na vihatarishi mbalimbali
inaonesha kwamba,utekelezaji wa sera ya fedha kwa kipindi cha Januari hadiJuni2024
umefanikiwa kudhibit mfumuko wa beina kubaki chini ya lengo la asilimia 5.
"Maamuzi ya Kamati pia yanazingatia mtazamo chanya wauchumi wa dunia, ambapo matarajio ni kuendelea
kupungua kwa mfumuko wa bei katika nchi nyingi, kuimarika kwa ukwasi katika masoko ya fedha duniani, na kushuka kwa beiza bidhaakatika soko la dunia.
Aidha, Kamatiinatarajia uchumi wa
ndanikuendelea kukua kwa kasi, sanjari na upatikanaji wa chakula chakutosha, na kupungua kwa kasi ya kushukakwathamani ya shilingi kufuatia ongezeko la mapato ya fedha za kigeni kutokana nashughuli zautalii, pamoja na mauzo ya dhahabu na mazao ya biashara na chakula.
"Katika kutathmini mwenendo wa uchumi wa dunia, Kamati ilibaini kuimarika kwa shughuli za kiuchumi katika nchi nyingi kwa robo ya kwanza na ya pili ya mwaka 2024.Mfumuko wa bei umeendelea kupungua, sanjari na kuimarikakwa ukwasi katika masoko ya fedha duniani, na benki kuu katika nchi nyingi kuanza kupunguza viwango vya riba.
"Bei ya mafuta ghafi ilipungua,
licha ya kuongezeka kidogo mwishonimwa mwezi Juni 2024. Bei ya dhahabu ilendelea kuwa juu, ikiashiriadhahabu kuendelea kutumika kamauwekezaji mbadala katika mazingra ya kushuka kwa thamani ya sarafu mbalimbali na migogoro ya kisiasa duniani.
"Matarajio ni uchumi wa duniakuendelea kuimarika katika kipindi kilichobaki cha mwaka 2024 na 2025, licha ya
kuwepokwahatari ya kuongezeka kwa migogoro ya kisiasana mizozo yakibiashara.
"Kuhusu mwenendo wa uchumi wa Tanzania, Kamati imeridhishwa na kuendelea kuimarika kwa shughuli za kiuchumi, kutokana na utekelezaji wa sera thabiti na maboresho mbalimbali yenye lengo lakukuza uchumi.
"Hali hii ya kuimarika kwa uchumi inatarajiwa kuendelea katika siku zijazo,
kufuatiahali nzuri ya hewa kwa ajili ya shughuli za kilimo, upatikanaji wa uhakika wa umeme, uboreshaji wa miundombinu (hususan reli, barabara, na bandari), pamoja na sera na programu za maboresho.
"Baadhi ya maeneo mahsusi ya mwenendo wa uchumi yaliyofanyiwa tathmini ni Uchumi ulikua kwa asilimia 5.1 mwaka 2023, ikilinganishwa na ukuaji waasilimia 4.7
mwaka 2022.
"Ukuaji huu ulichangiwa zaidi na shughuli zakilimo, uchimbaji madini na
mawe, ujenzina shughuli zakifedha (hususan ongezeko la mikopo kwa sekta binafs).
Aidha, shughuli za utalii, ambazo zinategemeana na sekta nyingine za uchumi
zimeendelea kuchangia kuimarika kwa uchumi nchini.
"Kamati inakadiria ukuaji wa uchumi
kuwa takriban asilimia 5 na 5.4, katika robo ya kwanza na ya pili ya mwaka 2024,
mtawalia. Vilevile, mwenendo wa uchumi wa Zanzibar umeendelea kuwa imara, ambapo
ulikuakwa asilimia 7.4 mwaka 2023, ikilinganishwa na asilimia 6.8 mwaka 2022.
Mwenendo huu unachangiwa kwa kiasi kikubwa nashughuli zautalii, huduma za chakula na uwekezaji kwenye sekta yaujenzi.
"Mwenendo huu wa ukuaji wa uchumi nchini
unatarajiwa kuendelea katka nusu ya pili ya mwaka 2024 na 2025.Mfumuko wa bei uliendelea kuwa tulivu na chini ya lengo la nchi la asilimia 5, na vigezo
vya utangamano vya kikanda kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
"Mwezi Aprili na Mei 2024, mfumuko wa bei ulikuwa asilimia 3 na 3.1, mtawalia. Mwenendo huu ulitokanana kupungua kwa mfumuko wa bei wa chakula kufuatiauwepo wa chakula cha kutoshanchini, pamoja na sera thabitiza fedha na bajeti. Kwa upande wa Zanzibar, mfumuko wa beiumeendelea kupungua hadi kufikia takriban asilimia 5, kutokana na kupunguakwa bei za chakula na bidhaa zisizo za chakula.
"Mfumuko wa bei unatarajiwakubaki ndani ya wigo wa asilmia 3-4, katika nusu ya pili ya mwaka 2024 na kuendelea, ikichagizwa na utekelezaji wa sera thabiti za fedha na bajeti, upatikanaji wa chakula cha kutosha, upatikanaji wa uhakika wa nishatiya umeme, na kushuka kwa bei zabidhaa katika soko la dunia.
"Kuendelea kuimarika kwa hali ya uchumi, kumechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji imara wa mikopo kwa sekta bnafsi na utulivu wa sekta ya fedha. Katika robo ya pili ya 2024, mikopo ya sekta binafsi inakadiriwa kukua kwa wastani wa asilimia 16.4 ikilinganishwa na asilimia 17.1 katika robo iliyotangulia. Sekta ya benki iliendelea kuwa na ukwasi na mtaji wa kutoshahuku ikitengeneza faida.
Aidha, amana, rasilimali na mikopo imeendelea kuongezeka.
"Ubora wa rasilmali za benki umeendelea kuimarika, kufuatia kupungua kwa
kiwango cha mikopo chechefu hadi asilimia 4.4 Mei 2024, ndani ya wigo unaokubalika wa chini ya asilimia 5,na asilimia 5.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2023.Mikopo kwa sekta binafsi inatarajiwa kuendelea kuongezeka katika kipindi kijacho cha mwaka 2024 kutokana na kuimarika kwa hali ya uchumi wa dunia na wa ndani.
"Utekelezaji wa bajeti ya Serikali umeendelea kuwa wa kuridhisha huku ukichagiza
utekelezaji wa sera ya fedha. Mapato ya ndani kwa Tanzania Bara yanakadiriwa kufikiaasilimia 95ya lengo. Kwa upande wa Zanzibar, mapato yanakadiriwa kuvuka lengo kwa asilimia 0.3 kutokana na maboresho katika usimamiz wa kodi na kuongezeka kwa utayari wa wananchi kulipakodi. Katika mwaka2024/25, Serikali inakusudia kutekeleza sera inayolenga kupunguza matumizi na kuendelea kutekeleza programu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ya Extended Credit Facility (ECF), pamoja na programu ya Resilience and Sustainability Facility(RSF).
Urari wa malipo ya kawaida uliendelea kuimarika, kuendana na kupungua kwa athari za mitikisiko ya kiuchumiduniani. Mauzo njeya nchiyaliongezeka kutokana na uuzaji wa dhahabu, mazao asiliana shughuli za utalii. Uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje uliongezeka japo kwa kiwango kidogo ikilinganishwa namauzo ya nje.
Hivyo, nakisi ya urari wa malipo ya kawaida (current account deficit) inakadiriwa kupungua hadi dola milioni 959.2 katika robo inayoishia Jun 2024 ikilinganishwa na dola milioni 977.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2023.
Kwa upande wa Zanzibar, urari wa malipo ya kawaida unakadiriwa kuwa ziada ya dola za Marekanimilioni 421.5 katika mwaka unaoishia Juni 2024, ikilinganishwa na ziada ya dola milioni 411.5 katika kipindi sawia cha mwaka 2023.
"Hali hii ilitokana na kuongezeka kwa mapato yatokanayo na huduma, hususan utalii. Nakisi ya urari wa malipo ya kawaida inatarajiwa kuendelea kupungua hadi asilimia 3.2 ya Pato la Taifa katika kipindi kilichobaki cha mwaka 2024.
"Akiba ya fedha za kigeni iliendelea kuwa yakutoshakwa kuwa na zaidi ya dola za Marekani bilioni 5, kasi kinachotosheleza uagizaj wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa zaidi ya miezi 4. Upatikanajiwa fedha za kigeni uliimarika kiasi, mwishonimwa mwezi Juni 2024, kutokana na ongezeko la fedha za kigeni kutoka kwenye mauzo ya tumbaku, dhahabu na shughuli za utalii.
"Matarajio ni kuongezeka zaid kwa fedha za kigeni nchini kupitiamapato yatokanayo na shughuli za utalii,mauzo ya madini, bidhaa asilia, na usafirishaji wa chakua kwenda nchi jiran. Matarajio ya kuimarika kwa hali ya uchumi wa dunia na kupungua kwa beiza bidhaa katika soko la duniapia yatachangiaongezeko hilo.
Aidha, Benki Kuu inatarajiwa kuongeza akiba yake ya fedha za kigeni kupitia ununuzi wa
dhahabu kutoka katika masoko ya ndani.


Comments
Post a Comment