'C' EST JESUS YA NANA MARIAM KUTOKA NOVEMBA 16

<div
"" border="0" data-original-height="990" data-original-width="1080" src="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgKsipYh0XJCvlJw7d2FgyJDUJhyphenhyphenKEht5drJIVgrZMcTZBke_hygHYH_u23_OZFnccxwC9cwF_EKT3yQn1-oTHXJHkfcFHRwrFB6dmteP8zMgGqiXOZSw6QJp9H-393PpvCKGGsjqaKbVjKv42a5p817SDKrW-m940X58mtvcKvT4igm-tQhcq5Hthv_Mfn/s1600/Screenshot_20251111-135419.png"/>
'C'est Jesus' ya Nana Miriam kutoka Novemba 16 MWIMBAJI anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Injili nchini Kongo, Nana Miriam ameachia kionjo cha wimbo mpya, C'est Jésus, alioshirikiana na Sylvain Kashila. Waimbaji hao ambao kwasasa ni tishio nchini Kongo, wameteka hisia za mashabiki wa muziki huo punde baada ga kuachia kionjo cha ngoma hiyo inayotarajia kutoka Novemba 16, mwaka huu. Akizungumzia kolabo hiyo Nana Miriam, amewataka mashabiki wa Afrika Mashariki na Kati wakae mkao wa kumtukuza Mungu kupitia wimbo huo uliowabariki wengi. "Wimbo unatoka wiki ijayo Novemba 16, naomba mashabiki zetu wa hapa Kongo, Tanzania na sehemu nyingine dunia wakae karibu na mitandao yetu ya kijamii ili video inapotoka waweze kutupa sapoti ili kolabo yetu hii C'est Jésus ifike mbali," amesema Nana.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA