STEVE NYERERE HESHIMU MAMLAKA UHURU WA MAONI UNA UKOMO
Anaandika @stevenyerere2 “Mheshimiwa Rais @samia_suluhu_hassan, hongera sana kwa ziara yako wilayani Meatu. Haiwezekani kila mtu akajiona ana haki ya kusema chochote, mahali popote, na wakati wowote. Watu wanasahau kuwa uongozi ni hekima, busara na uvumilivu – lakini kwa wajinga na wasioelewa, huona kama wako juu ya sheria.
Haiingii akilini mtu kusimama mbele ya Rais wake, mbele ya Mwenyekiti wake wa chama, na kusema anammdai. Huo siyo uungwana wala heshima.
Watu wa aina hiyo wapo wengi Mheshimiwa Rais, lakini leo umeonyesha sura yako halisi kama Kiongozi Mkuu wa nchi na Mwenyekiti wa Chama. Umeonyesha makali yako – hongera sana.
Ninaamini sasa watajipanga upya, lakini kamwe hawataweza. Tufike mahali tutambue kuwa kuna dola, kuna mamlaka, kuna serikali – hakuna aliye juu ya dola.
Huwezi kuzuiwa kusema, lakini hakuna uhuru usio na mipaka. Wamezidi sana!”– Steve Nyerere.


Comments
Post a Comment