WASANII WA MAMA ONGEA NA MWANAO NA LAMATA VILLAGE WAWA KIVUTIO KAMPENI ZA SAMIA

Wasanii wa mama ongea na Lamata Village wawa kivutio kampeni za Dkt. Samia
Wasanii kutoka makundi maarufu ya Mama Ongea na Mwanao pamoja na Lamata Village wameendelea kuwa kivutio kikubwa katika kampeni za Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutokana na ubunifu na kazi kubwa wanayoifanya mikoani. Makundi hayo yanayoongozwa na Steven Nyerere na Leah Lamata 'Lamata' yamekuwa chachu ya hamasa kila wanapofika kwenye mikutano ya kampeni, wakikonga nyoyo za wananchi kwa burudani na jumbe za mshikamano. Mashabiki wengi wamekuwa wakishangilia kwa nguvu kubwa kila mara wasanii hao wanapopanda jukwaani na kuhamasisha wananchi kumpigia kura Dkt. Samia, huku wakiahidi kumchagua ifikapo mwezi Oktoba. Kwa mujibu wa mashuhuda wa kampeni hizo, uwepo wa wasanii hao umeongeza mvuto na msisimko, hali inayochangia hamasa kubwa kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kampeni na mchakato wa uchaguzi. Mwisho

Comments