NABII MALISA AMSHUKURU DKT SAMIA KWA KURUHUSU HUDUMA ZA KIROHO

 


CHUNGAJI wa Kanisa la Madhabau ya Hatma, Nabii Clear Malisa, amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kwa serikali yake kwa kutoa uhuru wa kuabudu bila kuchagua.


Malisa ameyasema hayo mapema leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia mkesha mkubwa unaotarajia kufanyika leo kanisani kwake  Ubungo Kibangu.

"Rais Samia amekuwa na ushirikiano mkubwa kwetu viongozi wa dini, tunamshukuru kutobagua dhehebu lolote"amesema Malisa.

Hata hivyo, Malisa ameutabiri mwaka 2025 utakuwa mwaka wa neema zaidi kwa Taifa la Tanzania katika nyanja ya uchumi  ikiwemo kupanda kwa shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola za Kimarekani.

Pia ameongeza kwa kutoa utabiri anaofanya, kiongozi huyo kwa kiroho amesema ni Utashi ambao Mungu amempa na kuhaidi kutoa utabiri juu ya mambo mbalimbali ikiwemo uchaguzi mkuu wa hapo mwakani kupitia kwenye mkesha utakaofanyika kanisani leo.

Aidha Nabii  Malisa amewataka watanzania kipindi hiki cha mkesha huu wa mwisho wa mwaka kujitokeza kwenye nyumba za Ibada kufanya maombi na kumshukuru Mungu.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA