TRC YAOMBA RADHI HITILAFU NYINGINE YA TRENI


Shirika la Reli Tanzania (TRC)  imewaomba radhi abiria waliosafiri na treni ya kawaida  kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam Agosti Mosi,2024  kwa kuchelewa kuwasili kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyotokea.

Treni hiyo iliondoka Dodoma majira ya saa 2:15 usiku   na kupata hitilafu  katika  eneo la Mtaa wa Mshikanano, Kata ya Kihonda Mkoani Morogoro.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano ,Jamila Mbarouk ilieleza kuwa hitilafu za kiufundi zilitokea majira ya saa 4:33 usiku nakushughulikiwa  kwa muda wa takribani saa moja na kusababisha treni  hiyo ya abiria kutoka Dodoma kuchelewa kuwasili Dar Es Salaam kwa wakati uliopangwa. 

Aidha Shirika lilisema kuwa tremi iliyobeba viongozi na wananchi wengine  walitoka Dodoma saa moja usiku baada ya kushiriki sherehe za uzinduzi wa SGR waliwasili Dar es Salaam kwa muda uliopangwa bila hitilafu yoyote. 

“TRC inazingatia usalama wa abiria kabla na wakati wa safari ili kuepusha madhara kwa watumiaji  wa huduma za usafiri wa reli na lionaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza,”ilisisitiza taarifa hiyo.

Julai 30,2024 hitilafu ilitokea ya umeme katika stesheni ya Kilosa na Kidete  na kusababisha treni ya SGR  iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma  kusimama kwa muda wa saa mbili.

TRC iliwatajwa wanayama kama bundi na Ngedere kuwa kisababishi ya hitilafu wanapogusa nyaya  za umeme zilizotandazwa juu ya reli baada ya safari za treni hizo kuanza rasmi Julai 25,2024. 

Mwishoo…

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA