JONATHAN BUDJU AFUNGA MWAKA NA ITURI

Jonathan Budju afunga mwaka na 'Ituri Amani' Na Bright Davis Mwimbaji nyota wa Injili kutoka nchini Canada, Jonathan Budju, ameweka wazi kuachia wimbo mpya hivi karibuni maalumu kuhamasisha amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Budju amejizolea umaarufu mkubwa kwenye muziki wa Injili pamoja na kujihusisha na masuala ya kijamii kupitia taasisi yake ya JB Foundation inayofanya kazi Afrika Mashariki. Akizingumza na gazeti hili, Jonathan amesema wimbo huo utatoka Disemba 19, akiwa ameshirikiana na waimbaji wa Ituri Gospel Artist na utaitwa Itune Amani. "Lengo ni kuendelea kuhamasisha amani Mashariki mwa DRC maeneo ya Ituri na Kivu, naamini wimbo utagusa wengi na kubadilisha maisha yao, nitatoa video na audio kwa pamoja katika platforms zangu zote za muziki," amesema Jonathan.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA