KAJALA AFUNGUKA UKWELI KUHUSU LULU KUJITOA KUNDI lA BIG SIX

Kajala Afunguka: Ukweli wa Kuvunjika kwa Kundi la “Big Six” na Brighitter Msanii maarufu wa filamu nchini, Kajala Masanja, amefunguka na kuweka wazi ukweli kuhusu kuvunjika kwa kundi lao maarufu lililojulikana kama “Big Six”, lililowakutanisha wasanii wakubwa wa kike nchini.
Akizungumza kuhusu kundi hilo, Kajala amesema ni kweli walikuwa wasanii sita waliounda umoja huo, ambao ulihusisha Wolper, Aunty Ezekiel, Wema Sepetu, Kajala Masanja, Irene Uwoya na Elizabeth Michael (Lulu).
Kajala amesema mwanzo wa kuvunjika kwa kundi hilo ulianza pale Elizabeth Michael alipokuwa wa kwanza kujiondoa. Kwa mujibu wa Kajala, Elizabeth aliwaeleza wenzake kuwa alikuwa anatarajia kuingia katika maisha mapya ya familia.
“Elizabeth alituambia kuwa hivi karibuni anatarajia kuitwa mama, hivyo alihitaji muda mwingi kuwa karibu na mume wake na watoto wake,” amesema Kajala. Baada ya maelezo hayo, Kajala anasema wanakundi walikubaliana kumpa nafasi Elizabeth Michael ili ajikite kwenye familia yake.
Hata hivyo, Kajala ameendelea kueleza kuwa hali ilibadilika zaidi pale walipopanga safari ya pamoja ya vacation kwenda Zanzibar. Akiwa katika maandalizi ya safari hiyo, Wema Sepetu alimfuata Kajala na kumuuliza kama safari bado ipo.
“Nilimjibu kuwa maandalizi yanaendelea, lakini ghafla Wema alisema kuwa siku hizi hasikilizwi kwenye kundi letu, kisha akaondoka,” ameongeza Kajala.
Kajala amesema katika kipindi hicho, yeye na Wema hawakuwa na maelewano mazuri, hali iliyochangia mgogoro huo.
Baada ya tukio hilo, Wema Sepetu aliamua kujiondoa kwenye kundi lao la WhatsApp, jambo lililowashangaza wanakundi wengine. Wolper na Irene Uwoya walisema hawakuona Wema akijiondoa, huku Kajala akieleza kuwa naye aligundua baadaye kuwa Wema hayupo tena kwenye kundi.
Tofauti na wengine, Aunty Ezekiel alisema yeye alimuona Wema akijiondoa kwenye group hilo, jambo lililomfanya Wolper kwa utani kusema: “Basi itakuwa wewe Aunty Ezekiel ndiye Admin wa group.”
Kwa maelezo hayo, Kajala ameweka wazi kuwa kuvunjika kwa Big Six hakukutokana na chuki, bali mabadiliko ya maisha, kutokuelewana na maamuzi binafsi ya kila mmoja.
kwa sasa wamebaki Irene Uwoya, Aunty Ezekiel, Frida Masanja 'Kajala', Jacqueline Wolper

Comments