JENI AHUKUMIWA KWA KULA NAULI YA EMMA
Mahakama ya Mwanzo jijini Lagos nchini Nigeria, imemhukumu Mwanamke anayefahamika kwa jina la Jennifer kulipa faini ya ₦450,000 sawa na zaidi ya Shilingi laki 730,000 za Kitanzania baada ya kupatikana na hatia ya kupokea fedha kwa udanganyifu.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za Mahakama, Jennifer alipokea 30,000 sawa na Shilingi 490,000 kutoka kwa kijana aitwaye Emmanuel, aliyedai kumtumia fedha hizo kwa ajili ya nauli ya kumtembelea nyumbani kwake, hata hivyo, baada ya kupokea fedha hizo, Jennifer hakufika kama walivyokubaliana na baadaye akakata mawasiliano.
Emmanuel aliwasilisha malalamiko mahakamani, akieleza kuwa kitendo hicho kilikuwa ni aina ya utapeli wa kifedha, baada ya kusikiliza ushahidi, mahakama iliamua kwamba hatua ya Jennifer ilikuwa ni udanganyifu na unyonyaji wa kifedha, hivyo kumlipa Emmanuel fidia kubwa zaidi ya kiasi alichotapeliwa awali.
Hakimu aliyesikiliza shauri hilo alisisitiza kwamba visa vya utapeli wa nauli ya usafiri vimekuwa vikiongezeka na vinachukuliwa kama aina ya uhalifu wa kimtandao na aliongeza kuwa hukumu hiyo imelenga kuwa fundisho na onyo kwa wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Jennifer sasa anatakiwa kulipa faini ya ₦450,000, na endapo atashindwa kufanya hivyo, atakabiliwa na hatua zaidi za kisheria.

Comments
Post a Comment