HUYU SASA NDO NANDY AFRICAN PRINCESS WA BILlNASS

Africa Princess, muziki wake, tuzo, ndoa na muziki wake kimataifa Faustina Mfinanga anayefahamika kwa jina la Nandy ni mtunzi mwimbaji na Mwigizaji kutoka nchini Tanzania. Alizaliwa 9 Novemba 1992 mjini Moshi mikoani Kilimanjaro.
Nandy amejipatia umaarufu mkubwa katika muziki wa Bongo fleva kupitia uimbaji wake wa Afro Pop akijulikana kwa sauti yake ya kuvutia na uwezo wake kuwasilisha hisia kupitia nyimbo zake. Nandy alianza safari yake ya muziki akiwa mdogo, akiimba kwaya kanisani. Baadae alijiunga na bendi ya muziki ya B band ambapo alifanya Maonyesho pamoja na kuimba na msanii mkubwa Banana Zorro.
Mwaka 2017 alishiriki katika shindano la uimbaji ya Tecno Own Stage, ambalo lilimpa nafasi ya kushiriki katika Coke Studio Afrikawaka huo huo. Kupitia jukwaa hilo, alionheza umaarufu wake na kuanza kushirikiana na wasanii mbalimbali wa Kimataifa. Msanii Bora wa kike Afrika Mashariki mwaka 2017/2020 Tuzo Nandy ameshinda tuzo kadhaa za muziki ukiwa ni pamoja na All Africa Music Awards (AFRIMA) AMI Awards Africa Msanii Bora Chipukizi mwaka 2018. Africa Entertainment Awards, USA (AEAUSA) Msanii Bora wa kikewaka 2021.Tanzania Music Awards TMA mwaka 2021 alishinda tuzo tatu binafsi, ikiwa ni pamoja na wimbo Bora wa kushirikiana kupitia wimbo wa 'Loyalty'aliomshirikisha msanii wa hip hop Darassa
Nandy amefanya Collabo ushirikiano na wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania, akionyesha uwezo wake wa kubadilika na kupendana na mitindo tofauti ya muziki. Baadhi ya Collabo hizo ni Njiwa aliofanya na Msanii kutoka nchini Kenya Will Paul, Hallelujah, Kizaizai wimbo uliopendwa sana na mashabiki. Loyalty na Darassa ulioshinda tuzo ya wimbo Bora wa kushirikiana. Ameshirikiana pia na wasanii kama Sauti Soul na Joe boy, akionyesha uwezo wake wa kuvuka nje ya mipaka ya Tanzania.Nandy ni mwanzilishi wa tamasha linalojulikana kama Festival tamasha linalolenga kuonyesha na kukuza vipaji vya wasanii na kutoa burudani kwa mashabiki ndani na nje ya Tanzania. Tamasha hili limebahatika kufanyika katika mikoa mbalimbali ikiwemo kigoma na Dar es Salaam na limekuwa jukwaa muhimu kwa wasanii chipukizi na wakongwe kuonyesha vipaji vyao kupitia kazi zao.
Nandy ameolewa na Msanii wa Bongo fleva Wiliium Lyimo Billnass wamebahatika kupata mtoto mmoja mbali na muziki pia Nandy ni Balozi wa UNICEF na anajihusisha na biashara ya urembo kupitia vipodozi make up by Nandy na lipstick zenye nembo ya Nandy kama shuu.
Nandy ameendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika muziki wa kizazi kipya akichangia kukuza na kuendelea tasnia ya muziki wa Bongo fleva kimataifa kupitia sauti yake ya kipekee kushirikiana na wasanii mbalimbali juhudi zake katika kuandaa matamasha ameonyesha ni msanii mwenye dhamira ya ukweli kukuza na kutangaza muziki wa Bongo fleva ndani na nje ya nchi.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA