Ben Pol atoa wito kwa wasanii kuzingatia taratibu za Sanaa

Msanii nyota wa muziki wa R&B, Ben Pol, ametoa wito kwa wasanii wote kuhakikisha wanakuwa na kibali halali cha BASATA na kuendeleza utamaduni wa kutembelea Baraza la Sanaa la Taifa ili kujifunza zaidi. Ben Pol alitembelea ofisi za BASATA na kukutana na Katibu Mtendaji, Dkt. Kedmon Mapana, ambapo alihuisha kibali chake cha sanaa. Kupitia ziara hiyo, aliwahimiza wasanii kuhakikisha wanazingatia taratibu za kisheria na kusajili kazi zao rasmi ili kulinda haki zao na kuimarisha tasnia ya sanaa nchini. Akiipongeza BASATA kwa juhudi zake katika kukuza na kulinda sanaa Tanzania, Ben Pol alisisitiza kuwa ushirikiano mzuri kati ya wasanii na taasisi hiyo ni nyenzo muhimu kwa mafanikio ya sekta ya sanaa. Ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa weledi na pia kushirikiana na BASATA katika kukuza vipaji vya wasanii chipukizi, akihamasisha utii wa sheria na ubunifu wenye maadili.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA