TANESCO YAZINDUA NAMBA MPYA KWA HUDUMA BORA KWA WATEJA


Wapokeaji simu wa TANESCO wametakiwa kutoa majibu mazuri kwa wateja ili kuboresha huduma kwa Watanzania. Serikali imesisitiza kuwa haitavumilia huduma zisizokidhi mahitaji ya wananchi.

Katika juhudi za kuboresha huduma kwa wateja, TANESCO imezindua namba mpya ya simu 180, ambayo ni bure kupiga kwa mitandao yote isipokuwa mtandao wa Yas, ambao bado uko kwenye marekebisho ya huduma zao.


Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema kuwa namba ya awali iliwakwamisha wananchi wengi kutoa taarifa kwa sababu ya ukosefu wa salio. "Kwa sasa, kupitia 180, wateja wanaweza kutoa taarifa na kutatua changamoto zao bila malipo," alisema Kapinga.

Pia, Naibu Waziri amesisitiza kuwa serikali inaendelea kutekeleza mpango wa kuboresha upatikanaji wa umeme nchini katika maeneo mbalimbali. "Umeme utasaidia siyo tu katika shughuli za nyumbani kama kupika kwa haraka na usafi, bali pia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi," aliongeza.

Hatua hii inatarajiwa kuboresha huduma kwa wananchi na kuhakikisha changamoto za umeme zinatatuliwa kwa haraka.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA