LAMATA KUWAUNGANISHA KAJALA NA HARMONIZE
Penzi la Kajala na Harmonize lamata kuwaunganisha
Mtayarishaji wa filamu Leah Mwendamseke 'Lamata' amefunguka juu ya sababu ya kuwakutanisha msanii wa filamu nchini Frida Kajala na msanii wa Bongo Fleva nchini Rajab Abdul 'Harmonize'.
Wawili hao, ambao hapo awali walikuwa wapenzi hadi walifikia hatua ya kuvalishana pete, lakini mahusiano yao yalikatishwa njiani na wakaishia kutupiana maneno mitandaoni, walifanikiwa kukutana tena uso kwa uso katika mechi za Samia Cup zinazoendelea.
Lamata amesema, "Kweli nilikuwa kiunganishi cha wawili hao kwa kuwa wote ni watu wangu wa karibu, hivyo wakawa pamoja. Yalioendelea baada ya hapo ni yao wenyewe."
Mbali na hilo, Lamata ameongelea pia maendeleo ya timu yake, Lamata Village SC, akieleza safari yake tangu mwanzo wa mawazo yake hadi leo ambapo timu hiyo inapata Shilingi Milioni 5 kutoka Selcom.
"Nilianzisha timu ya Lamata Village kama utani, lakini naona wakiendelea kufanya vizuri hadi kufikia hatua ya kushinda kiasi cha Shilingi Milioni 5 sio jambo dogo," amesema Lamata.

Comments
Post a Comment