TUZO ZA KARIAKOO BUSINESS AWARDA KUKUZA USHINDANI WA BIASHARA
Mwandaaji wa tuzo hizo, Frank Mbwana, amesema lengo la tuzo hizo ni kutambua mchango wa wafanyabiashara wa Kariakoo na kuwapongeza kwa juhudi zao katika kukuza uchumi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka Watanzania kuwaunga mkono wafanyabiashara wa Kariakoo na kushirikiana nao kwa maendeleo ya biashara nchini.
"Tuzo hizi zimekuja wakati muafaka na katika sehemu muhimu ya biashara. Sikutarajia kuona muitikio mkubwa wa wafanyabiashara," alisema Mpogolo.
Naye Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Kumbilamoto, amepongeza mshikamano wa wafanyabiashara wa Kariakoo na juhudi zao za kuendeleza biashara.
Kwa upande wake, Seveline, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, amepongeza kuanzishwa kwa tuzo hizo, akisema zitachochea ushindani wa kibiashara na kuongeza ufanisi katika sekta hiyo.



Comments
Post a Comment