LYDIA AELEZEA SAFARI YAKE YA KUSAIDIA MABINTI

Mkurugenzi Mtendaji wa herinitiative Lydia Charles akielezea lilipotokea wazo la kuwasaidia mabinti kutoka chini na kwenda ngazi za juu kijamii, kisiasa na kiuchumi “Siku moja, nikiwa safarini kwenda Dodoma, nilisimama barabarani kupata kifungua kinywa, Msichana mdogo aliniletea supu. Nilimuuliza, Kwa nini hauko shuleni au nyumbani? Alinijibu, Ningetamani iwe hivyo, lakini niko kwenye hali ngumu sana.”
“Maneno ya yule msichana yalinifanya nitafakari, Kuna wasichana wengi wenye ndoto kubwa, lakini umasikini ni kikwazo kikubwa, Nikakumbuka hadithi yangu mwenyewe, safari yangu kutoka shule ya kata isiyo na maktaba, maabara, wala walimu wa kutosha” “Shule yangu ilikuwa na changamoto nyingi masaa mawili ya kutembea kila siku, wanafunzi wengi wakiacha shule kwa sababu ya umasikini, ndo
a za utotoni, na mimba za mapema, Tulianza 200, lakini ni 9 tu tulifika kidato cha sita, 3 tu tukiwa wasichana” “sikuwa na Uwezo mkubwa lakini nilihitaji kufanya kitu, Mimi na marafiki zangu wawili tukaanzisha Teen Girls Support Initiative kusaidia kujenga kujiamini na kuelewa haki za wasichana mpaka sasa Tumesaidia wanafunzi 1,000+ katika shule 10.”- Lydia Charles , Executive Director / @herinitiative

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA