Waitara NBC Trophy yavuta wachezaji 147

MWENYEKITI wa Klabu ya Gofu Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu Michael Luwongo amesema shindano la Waitara NBC Trophy limepata mafanikio baada ya kuwavutia wachezaji 147 kujitokeza kushiriki katika vipengele tofauti. Kivutio kikubwa zaidi katika shindano hilo ni aliyeshinda ushindi wa jumla ni Mtu mzima kidogo kwa mara a ya Mzee ukilinganisha na idadi kubwa ya washiriki ni vijana. Mshindi wa jumla alikuwa Dk Edmund Mndolwa ambaye alipata pointi za juu akishinda Gross 78 HCP 12 na Net 66 ambaye hata yeye mwenyewe hakuamini na kusema atawaonesha wajukuu zake Kombe alilopata. Luwongo amesema shindano hilo la kumuenzi Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara lilikuwa lifanyike mwaka jana lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao hawakufanikiwa na ndio lilifanyika mwishoni mwa wiki huku akitangaza lingine litafanyika tena hapo baadaye. "Tumepata mafanikio kwasababu washiriki wamekuwa wengi katika vipengele lakini mwisho wa siku washindi ni wachache, tunawapongeza wote walioshiriki wakiwemo watoto, vijana, wanawake na wazee,"amesema. Jenerali Waitara ni muasisi wa klabu ya Gofu ya Lugalo na ndiye aliyeanzisha Viwanja vya kuchezea Gofu vya Lugalo hivyo wamekuwa wakimuenzi kwa shindano kila mwaka kuthamini mchango wake katika michezo nchini. Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA