PROF MORI AWAITA WADAU WA KIMATAIFA UWEKEZAJI WANAWAKE BENKI YA CRDB IKISHIRIKI MKUTANO NCHINI URENO

Profesa Mori awaita wadau wa kimataifa uwezeshaji wanawake Benki ya CRDB ikishiriki mkutano nchini Ureno
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Profesa Neema Mori ameshiriki mjadala wa Wanawake katika Biashara na Mitandao ya Ugavi uliofanyika pembezoni mwa mkutano wa Shirika la Fedha (IFC) wa Washirika wa Kimataifa wa Biashara unaondelea katika Jiji la Lisbon nchini Ureno.
Katika mjadala huo, Profe Mori amebainisha kuwa uwezeshaji wa wanawake ni sehemu ya mkakati wa muda wa kati wa Benki ya CRDB katika kiuchumi, akieleza kuwa Benki imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 800 kufadhili biashara zinazoongozwa na wanawake. Uwezeshaji huu ambao umewafikia wanawake zaidi ya milioni 1 kote nchini, amesema unafanyika kupitia suluhisho bunifu kama CRDB Malkia, pamoja na programu jumuishi zinazotekelezwa na CRDB Bank Foundation kupitia Program ya IMBEJU, zinazojumuisha elimu ya fedha, mafunzo ya ujasiriamali, na kuwaunganisha wanawake na fursa za kimasoko.
Aidha, amesisitiza juhudi za Benki katika kufungua masoko mapya kwa wanawake ikiwamo kuwawezesha kunufaika na fursa za biashara za kikanda na Soko Huru la Afrika. Haya yanaenda sambamba na uwekezaji katika sekta muhimu kama kilimo, biashara, na miradi endelevu ya kijani pamoja na miradi ya nishati safi ya kupikia inayohakikisha wanawake wanakuwa sehemu ya uchumi unaojali mazingira na maendeleo ya baadaye.
Ushiriki katika mkutano huo, unaeendelea kuonesha nafasi ya Benki ya CRDB kama kinara wa ajenda ya ujumuishi wa kiuchumi kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa mitaji, kujenga uwezo wa biashara, na kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika biashara za kimataifa na kukaribisha wadau kushirikiana na Benki. Profesa Mori amesema kupitia ubunifu, ushirikiano na uwekezaji wenye tija, Benki ya CRDB inaendelea kufungua milango ya mafanikio kwa wanawake Tanzania na barani Afrikavkwa ujumla.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA