JONATHAN BUDJU KAJA WIMBO MPYA 'SAFE IN YOU'
Jonathan Budju aibuka na wimbo mpya ‘Safe In You’
DAR ES SALAAM:STAA wa muziki wa Injili anayeishi Canada, Jonathan Budju, amewataka mashabiki wake kujiandaa na ujio wa wimbo wake mpya unaoitwa Safe In You, unaotarajiwa kugusa nyoyo za wengi.
Msanii huyo ambaye mapema mwaka huu alifanya vizuri kwenye chati za muziki wa Injili kupitia wimbo wake sifa zake, sasa amekamilisha maandalizi ya kazi yake mpya ikiwemo audio pamoja na video yenye ubora wa hali ya juu.
Akizungumza AMONLINE ujio wa wimbo huo, Jonathan amesema kuwa Safe In You utaachiwa rasmi Machi 27 kupitia majukwaa yote ya kidijitali, huku pia ukitarajiwa kuanza kuoneshwa kwenye vituo vikubwa vya televisheni Afrika Mashariki na Kati.
“Niliachia EP mwezi Januari ambayo imefanya vizuri sana kwenye mitandao. Nawashukuru mashabiki wangu na nawaomba waendelee kuwa tayari kupokea Safe In You, wimbo wenye ujumbe wa nguvu za Mungu utakaowabariki wengi,” amesema Jonathan.
Wimbo huo unatajwa kuwa na ujumbe wa matumaini, imani na faraja kwa wasikilizaji, ukiwaendeleza mashabiki wake katika safari ya kiroho kupitia muziki wake.
Mwisho


Comments
Post a Comment