KAMATI YA BUNGE YA MIUNDO MBINU YATAKA MRADI WA CHUO CHA ANGA KUKAMILIKA KWA WAKATI MASLAI YA WATUMISHI YALINDWE
DAR ES SALAAM:KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu imeishauri serikali kusimamia kwa ukamilifu mradi wa ujenzi wa Chuo Cha Usafiri wa Anga (CATC) kwani kukamilika kwake kuna kuwa na Tija na Manufaa kwa Taifa.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso wakati kamati hiyo ilipotembelea ujenzi wa Chuo Hicho kilichopo chini ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na kuongeza kuwa wahakikishe mkandarasi analipwakwa wakati ili atekeleza majukumu yake.
Aidha Kakoso ameshauri watanzania wachangamkie fursa ya kusomea kwani ina uhitaji mkubwa wa soko kwa sasa ukilinganisha na kipindi cha nyuma .
Naye Waziri Wa Ujenzi Makame Mbarawa amesema kozi zinazofundishwa katika chuo hicho si kozi awali ni kozi fupifupi hivyo kozi za awali bali ni zinafundishwa katika Chuo cha Usafirishaji ( NIT).
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Salim Msangi amesema mradi wa chuo hicho umegharimu bilioni 78 na hadi sasa wamemlipa mkandarasi asilimia 6.7 huku akisema kukamilika kwa chuo hicho kitaongeza uwezo wa kuwajengea wataalam uwezo hapa nchini.




Comments
Post a Comment