MUFTI AWATAKA WAISLAM KUENDELEZA MEMA HATA BAADA YA RAMADHAN
Mufti Awataka Waislam Kuendeleza Mema Baada ya Ramadhan
DAR ES SALAAM
Waislam nchini wametakiwa kuendeleza matendo mema waliyojifunza na kuyatekeleza katika kipindi cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, hata katika miezi 11 ijayo, ili kudhihirisha uhalisia wa ibada na maadili waliyojijengea wakati wa mwezi huo.
Wito huo umetolewa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally, wakati akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB.
Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake, Mufti aliwaasa Waislam kujitathmini na kujiuliza kama wataweza kuendeleza matendo mema waliyokuwa wakiyafanya katika mwezi wa Ramadhan hata baada ya kumalizika kwa mwezi huo mtukufu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Nsekela, amesema kuwa futari hiyo ni sehemu ya kutoa shukrani kwa wateja wa benki hiyo ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio yake na kuifanya kuendelea kuwa miongoni mwa benki bora nchini Tanzania.






Comments
Post a Comment