WAISLAM WATAKIWA KUENDELEZA MATENDO MEMA KAMA ILIVYOKUWA RAMADHANI

Waumini wa dini ya kiislamu wametakiwa kuishi kama walivyokuwa wanaishi kwenye mwezi mtukufu
SHEKHE Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Omari amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuyaenzi yale yote waliyoyafanya katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kuendelea kutenda yale mazuri na kuachana na maovu.
Ameyasema hayo leo Machi 22, 2026 wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Michezo (Mama Samia Orphans Eid Day Out) lililoshirikisha watoto wenye mahitaji maalum (Yatima) kwenye viwanja vya gofu Lugalo Dar es Salaam.
"Waislamu wanatakiwa kuishi kama walivyokuwa wanaishi katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi ambao umetukumbusha namna ambavyo tunatakiwa kuishi kwa kutenda mema na kuachana na yale maouvu," amesema Omari.
Amesisitiza waumini hao waishi kwa kusaidiana, kusameheana pamoja na kufanya ibada usiku na mchana kama kama ilivyokuwa katika mfungo huo. Ameipongeza Kampuni ya Chocolate Princess kwa kuandaa Tamasha hilo la kiimani pamoja na wadhamini wote wanaoguswa na watoto hao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Chocolate Princess Limited Mboni Masimba amesema amekuwa akitoa misaada mbali mbali kwa watoto yatima kipindi kirefu, na kudai ametoka kwenye kufuturisha na kuamua kuandaa Tamasha hilo lililoshirikisha watoto zaidi ya 1000 kutoka vituo 13.
Amehimiza watoto hao wasiwadharau walezi wanaowalea na badala yake wawaheshimu ili wapate baraka kutoka kwao, ikiwemo kufanya ibada.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA