KAMATI YA BUNGE:NIT KUONGEA UJUZI KWA WANAFUNZI UBORA WA CHUO KWA KUJITANGAZA
Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi chuoni hapo, Machi 16, 2026 Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Seleman Kakoso, amesema kuwa endapo mfumo wa utoaji mafunzo utaimarishwa vizuri, wanafunzi wa chuo hicho watapata ujasiri zaidi wa kujieleza na kutumia ujuzi wao kwa vitendo.
Amesema kuwa pamoja na umuhimu wa ubunifu katika kuboresha elimu, chuo hicho kinapaswa pia kushughulikia changamoto mbalimbali zinazotokana na kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma katika taasisi hiyo.
Kwa mujibu wa Kakoso, ongezeko la wanafunzi linaweza kuleta ugumu katika usimamizi wa miundombinu na huduma muhimu kama vile vyoo, madarasa na huduma nyingine za msingi kwa wanafunzi.
“Chuo hiki ni kikubwa na kina wanafunzi wengi, lakini changamoto yake ni kwamba kadri wanafunzi wanavyoongezeka, inakuwa vigumu ‘ku-maintain’ miundombinu iliyopo. Hii inaweza kusababisha vyoo kuwa vichache na hata madarasa kutotosheleza mahitaji,” amesema.
Aidha, ameishauri taasisi hiyo kuongeza juhudi katika kutoa matangazo na kufanya kampeni za kuitangaza ili ijulikane zaidi ndani na nje ya nchi, jambo litakalosaidia kuvutia wanafunzi na wadau mbalimbali wa sekta ya usafirishaji na miundombinu.


Comments
Post a Comment