RAZACK AONDOKA NA MILIONI 30 ZA BSS NA KIWANJA
Msimu wa 14 wa BSS ulikuwa safari ya kusisimua yenye mshangao na vipaji vya kipekee. Licha ya ushindani mkubwa, Razack Adam kutoka Arusha alijitokeza kama nguzo imara ya ujuzi wa muziki. Sauti yake yenye nguvu na uwasilishaji wa kuvutia uliteka hisia za majaji na mashabiki kwa pamoja.
Razack amefanikiwa kuondoka na taji la ushindi pamoja na zawadi nono ya TZS milioni 30 baada ya kuingia tatu bora na King David pamoja na Frank, kisha fainali na King David aliyeshika nafasi ya pili msimu huu.Kwa kutwaa ushindi huo, Razack Adam ameandika historia kwa kuwa mshindi wa kwanza wa BSS kuwakilisha mkoa wa Arusha, akiacha alama yake kwenye muziki na kuinua heshima ya eneo lake.Jukwaa hili la Bongo Star Search (BSS), limeendelea kujizolea umaarufu mkubwa kwa kuchangia katika kuimarisha ujuzi na kuibua vipaji vya muziki kutoka maeneo tofauti ya Tanzania.



Comments
Post a Comment