TARURA KUANA KUJENGAMBEYA BRIDGE

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inatarajia kuanza usanifu wa daraja la kudumu la chuma (Mabey Bridge) litakalojengwa ili kuunganisha vijiji vya Nyali na Nzumbo katika kata ya Ulaya-Mikumi Wilayani Kilosa.


Hayo yameelezwa  Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff wakati akiongea na wananchi wa kata hiyo kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua hali ya miundombinu wilayani Kilosa.


“Nitawatuma wataalamu wangu wa TARURA Makao Makuu waje wafanye usanifu wa ujenzi wa daraja la kudumu la chuma ili kuunganisha vijiji hivi vya Nyali na Nzumbo”. amesema Seff 


Pamoja na hilo, amemwelekeza Meneja wa TARURA Mkoa wa Morogoro kuanza mara moja ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu (Kiteputepu) ili wananchi wa vijiji hivyo waendelee kupata huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi.


Vile vile Mhandisi Seff ameelekeza kufanyika kwa tathimini ya uharibifu wa barabara za Mikumi  ili ziwekwe kwenye mpango wa dharura wa kurudisha mawasiliano haraka iwezekanavyo.


Awali, Mbunge wa Jimbo la Mikumi ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge - TAMISEMI,Dennis Londo amesema barabara nyingi za Jimbo la Mikumi  zimeharibika vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuiomba  TARURA kuangalia uwezekano wa kukarabati hasa barabara za Kivungu-Kilangali Km. 1.5, barabara ya Miyombo-Dodoma Isanga Km. 10 pamoja na ujenzi wa daraja la kudumu la Nyali-Nzumbo.


Daraja la watembea kwa miguu katika mto Nyali ambalo linaunganisha  vijiji vya Nyali na Nzumbo litajengwa kufuatia lile la awali kuvunjika.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA