WAKAMATWA WAKISAFIRISHA BANGI
Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limefanikiwa kukamata gari ndogo aina ya Noah yenye namba za usajiri T 777 CBC ikiwa inasafirisha na magunia Kumi yakiwa na dawa za Kulevya aina ya Bhangi.
Gari hiyo imekamatwa katika eneo la Kijiji cha Chamgata Kata ya Kalemela Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Dereva wa gari hilo alitelekeza gari hiyo pembezoni mwa barabara ya Mwanza - Musoma na kutokomea kusikojulikana na jitihada za kumtafuta bado zinaendelea.

Comments
Post a Comment