BANKI YA CRDB IMEZINDUA MSIMU WA TATU WA SIMBANKING


Katika jitihada zake za kuhamasisha  matumizi ya mifumo ya kidijitali nchini, Benki ya CRDB imezindua msimu wa tatu wa kampeni ya ‘Benki ni SimBanking’ na kutenga jumla ya zawadi zenye thamani ya Shilingi milioni 470 mamilioni kwa wateja wake mwaka huu.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul amesema lengo la kampeni hiyo ni kujenga utamaduni wa matumizi ya kidijitali katika huduma za kifedha ili kuendana na kasi ya maendeleo na kuondokana na matumizi ya fedha taslimu.

“Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaihamisha dunia kutoka kwenye miamala ya fedha taslimu kwenda ile isiyohusisha fedha taslimu yaani cashless economy. Tanzania hatupaswi kuachwa nyuma, ni lazima twende na mabadiliko hayo tena kwa kasi inayostahili,” amesema Bonaventure.

Kushiriki na kujiwekea nafasi ya ushindi katika kampeni hiyo mteja anatakiwa kutumia SimBanking kufanya miamala yake yote ya kibenki ikiwamo kulipia ankara za maji, umeme au visimbusi vya television, ada, malipo ya manunuzi, kutuma pesa, kulipia kodi, mikopo ya kidijitali, kutoa fedha kwa ATM au CRDB Wakala, kulipia bima ya vyombo vya moto, na huduma nyenginezo.

“Kwa kadri mteja atakavyokuwa akifanya miamala mingi zaidi ndivyo atakavyojiwekea nafasi ya ushindi,” amesema Bonaventure huku akibainisha kuwa katika kampeni hiyo itakayoenda hadi mwisho wa mwaka, kutakuwa na washindi wa gari aina ya Nissan Dualis watakaopatikana kila baada ya miezi mitatu, huku zawadi za  bajaj na pikipiki zikitolewa kwa mshindi wa kwanza na wa pili kila mwezi.

Aidha, katika msimu huu wa tatu wa kampeni ya ‘Benki ya SimBanking’, Benki ya CRDB imetenga zawadi za kompyuta mpakato kufikia 10 kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu, zawadi za simu janja, pamoja na fedha taslimu.

Pamoja na zawadi hizi Benki hiyo pia imetenga kiasi cha Shilingi milioni 200 zitakazotolewa kupitia Tembo Points ambazo mteja atakuwa akikusanya kila anapofanya muamala. Wateja wataweza kubadili Tembo Points zao kuwa fedha na kuzitumia kulipia huduma au bidhaa.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA