MADAKTARI 12 WATANZANIA WAENDA KUTOA HUDUMA YA AFYA ZAMBIA

Serikali ya Tanzania imetuma madaktari bingwa 12 kwenda nchini Zambia kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo kwa watoto hii ikiwa ni sehemu ya kuendelea kutanua wigo wa tiba utalii na kukuza mahusiano baina ya nchi hizi mbili.






Wataalamu hao kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) ambao watakaa nchini humo kwa wiki mbili wanatarajiwa kutoa matibabu ya upasuaji mkubwa wa magonjwa ya moyo hususani kwa watoto chini ya miaka 15 na kuisaidia nchi ya Zambia kuanzisha huduma ya matibabu ya moyo nchini humo.

Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Afya, DR Mollel wakati akizungumza na vyombo vya habari juu ya huduma za mkoba (outreach services) za matibabu ya kibingwa nje ya Tanzania kutoka JKCI.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA