MISS KINONDONI YAANZA RASMI MILANGO IPO WAZI
KAMPUNI ya Queen J Investment imehimiza wasichana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki Miss Kinondoni 2024.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Miss Kinondoni Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Queen Johnson amesema fainali za shindano hilo zitafanyika Mei 11 mwaka huu kusaka washindi watakaowakilisha kwenye taji la urembo la Taifa.
"Tumefungua rasmi pazia kwa wasichana wanaotaka kuwania taji la urembo Kinondoni wajitokeze kujiandikisha ili kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania taji la urembo."
Amefunguka na kusema kwa muda mrefu wamekuwa ni wadau wa shindano la Miss Tanzania na kuwashukuru Kampuni ya The Look Kwa kuwapa jukumu mwaka huu kuandaa shindano hilo kwa mara ya kwanza.
Amefunguka na kusema kwa muda mrefu wamekuwa ni wadau wa shindano la Miss Tanzania na kuwashukuru Kampuni ya The Look Kwa kuwapa jukumu mwaka huu kuandaa shindano hilo kwa mara ya kwanza.
Nae Afisa Mwandamizi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Agustino Makame amefafanua kuwa mashindano hayo ni fursa kubwa kwa wasichana na serikali inayatambua kwani yamekuwa yakitoa watu wengi mashuhuri na viongozi.
Pia ametoa rai kwa wasichana wenye sifa za kuwania taji hilo kuchangamkia fursa huku pia, akihimiza wadau, makampuni wajitokeze kwa wingi kuwasapoti waandaaji hao ili kufanikisha.
Kinondoni ina historia ya kutoa warembo katika taji la Miss Tanzania kwa vipindi tofauti na miongoni mwao ni Wema Sepetu mwaka 2006, Nancy Sumari mwaka 2005, Faraja Kota 2004, Richa Adhia mwaka 2007, 2018 Queen Elizabeth na wengine wengi.


Comments
Post a Comment