FCS, VODACOM KUDHAMINI WIKI YA AZAKi
Shirika la Foundation for ¹Civil Society (FCS) na Vodacom Tanzania Foundation wamesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya shilingi Milioni 150, kwa lengo la kudhamini Wiki ya AZAKi 2024 itakayofanyika mwezi Septemba mwaka huu jijini Arusha.
Akizungumza mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge amesema fedha hizo kutoka Vodacom Tanzania Foundation, zimeongeza chachu ya ushirikiano katika kukuza maendeleo ya jamii kupitia Wiki ya AZAKi.
Katika kufanikisha Wiki ya AZAKi, FCS wamechangia shilingi Milioni 250 ambapo michango mingine inatoka kwa wadau wa maendeleo zikiwemo asasi za kiraia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Foundation Tanzania, Zuweina Farah amesema ili kufanikisha dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, ushirikiano wa pamoja unahitajika kati ya AZAKi, sekta binafsi na Serikali.
Kauli mbiu ya Wiki ya AZAKi kwa mwaka huu ni sauti, maono na thamani.

Comments
Post a Comment